• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MAAGIZO YA RC SINGIDA YATEKELEZWA NI KUHUSU KILIMO CHA UMWAGILIAJI ITAGATA ITIGI

Posted on: October 23rd, 2021

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge  akizunguza na Wananchi wa Kijiji wa Itagata hivi karibuni kuhusu umuhimu wa kilimo cha umwagiliji  na mikakati ya kurejesha skimu ya Umwagiliaji ya Itagata ambayo imegharimu kiasi sh shilingi Bilioni 2.2.

MATUMAINI ya kurejea kwa kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Itagata iliyopo wilayani Itigi mkoani Singida yameanza kujitokeza kwa Wakulima baada ya kuanza kutekelezwa kwa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ya kuvunja uongozi uliokuwepo na kuchukuliwa kwa mashamba ambayo hayaendelezwi katika skimu hiyo.

Ikiwa ni mwezi mmoja umepita baada ya mkuu wa mkoa kutembelea skimu hiyo na kuwataka wakulima kuchagua uongozi mpya ambao utashirikiana na viongozi mbalimbali kufanya tathmini ya ugawaji na uendelezaji wa mashamba, Oktoba 22, 2021 kwa mara nyingine ametembelea skimu hiyo na kukuta wamechagua viongozi wapya na tathmini ya mashamba imefanyika.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wakulima hao Mahenge amemshukuru mkuu wa wilaya hiyo, Rahabu Magesa na viongozi wengine kwa kuanza kutekeleza maagizo yake na kuwaeleza kwamba hatua hiyo iwe endelevu na kuhakikisha wakulima wanafuata sheria na taratibu za skimu hiyo.

“Skimu hiyo iligharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.2 tokea ilipoanza kujengwa mpaka mwaka 2019 ilipokabidhiwa kwa kijiji husika, ni lazima lazima usimamizi ufanyike ili uzalishaji uongeze iweze kutoa mchango kwa taifa” alikaririwa Dkt. Mahenge.

Aidha Dkt. Mahenge akiwa kijijini hapa akatoa wito kwa wakulima wote wenye umiliki wa mashamba katika skimu hiyo kulipa ada zinazotakiwa ambazo zitatumika kukarabati miuondombinu ya skimu pale itakapo hitajika.

Hata hivyo Rc huyo alisema ulinzi wa miundombinu ya skimu ni jukumu la kila mwananchi hivyo akawakumbusha watu wenye makazi ndani ya Skimu kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa kwenye skimu hiyo kama wakishindwa watalazimika kuhama.

Aidha maagizo hayo yametokana na malalamiko yaliyowasilishwa na Afisa Kilimo kwamba wakazi hao wamekuwa wakiwatishia wakulima wengine wakidai eneo hilo lipo chini yao jambo ambalo limeleta kero kwa wakulima wengine.

Akijibu maswali ya wananchi ambao wametakiwa kulipia ada wakati mashamba yao hayajafikiwa na miundombinu ya umwagiliaji na kufanya kilimo chao kutengemea mvua za msimu Mahenge akaendelea kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha miundombinu inatengenezwa maeneo yenye changamoto ya kufikisha maji ili wakulima waweze kumwagilia .

“Nataka tuelewane kwamba kila mkulima ndani ya skimu anahaki sawa na mkulima mwingine hivyo kila mtu anatakiwa kufikiwa na maji na kutoa ada kulingana na ukubwa wa anachokimiliki”.aliendelea kufafanua Mahenge.

DC wa wilaya hiyo Rahabu Mwagisa alisema kwa sasa wakulima hao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji ila Serikali inaendelea kuwaunganisha na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha ili kupata mikopo

Rahabu akawashauri wakulima hao kulima mpunga kwa kuwa soko lake ni la uhakika na watakao amua kulima matunda au mbogamboga wahakikishe wanalima kwa wingi kwa ajili ya kulitosheleza soko.

Awali Afisa kilimo wa kijiji cha Itagata Bi. Halima Issingo alibainisha kwamba skimu hiyo ina ukubwa wa ekari 400 zinazofaa kwa kilimo na inauwezo wa kulisha wilaya nzima endapo itafanya kazi kwa viwango vyake vyote.

Afisa kilimo huyo alisema jumla ya ekari 209 kati ya 400 zimegawiwa kwa wanachama na kati hizo ekari 115 ndizo zililzolimwa mpunga na kutoa tani 120.75 wakati ekari 26 zililimwa mahindi na kutoa tani 14.4

Alisema moja ya mipango ndani ya skimu ni kufikisha miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo ambayo hayana ili kuifanya skimu nzima iweze kuzalisha vya kutosha.

Wakulima nao wakapata nafasi ya kutoa maoni baada ya mkutano ambapo Musa Saidi mkulima wa skimu hiyo wameishukuru Serikali kwa hatua walioichukua ya kuhuisha skimu hiyo na kuomba wataalamu waendelee kutoa elimu kwa wakulima ili kubadilisha mazingira ya uzalishaji na kulima ki biashara.

Michaeli Simuli Ngawe mkulima wa mpunga naye akiomba Serikali kuwaletea mbolea na mbegu za kisasa za mpunga kwa kuwa wengi wao hawatumii mbolea na mbegu bora kwa kuwa dhamiara ya serikali na wakulima kwa sasa ni kubadilisha kilimo kiwe chenye tija.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni   Rahabu Mwagisa (aliyesimama) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Itagata hivi karibu. Mkutano huo ulihusu uhuishaji wa skimu ya umwagiliaji ya Itagata  ambayo serikali imetumia fedha nyingi lakini haitumuiki ipasavyo.

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Itagata wakisikiliza maagizo ya mkuu wa mkoa kuhusu uboreshaji wa skimu ya Itagata.

Mkuu wa mkoa akisikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wakulima wanaotumia skimu ya Itagata mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.