Serikali ya Mkoa wa Singida imewaagiza Waganga Wakuu wa Halmashauri za Wilaya mkoani humo kuhakikisha wanapanga Wauguzi na Watalaamu wa afya kada nyingine wa kutosha ambao watashirikiana na Madaktari Bingwa na Bobezi 40 wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika utoaji wa huduma mbalimbali za kiafya mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, ametoa kauli hiyo wakati akiwakaribisha madaktari bingwa na bobezi wa Rais Samia ambao wamekuja mkoani Singida kusaidia matibabu ya kibingwa na bobezi kwa wananchi wa mkoa wa huo kwa muda wa Siku Sita (6) kuanzia leo tarehe 13 Mei hadi 18 Mei, 2024.
Katibu Tawala huyo amesema kazi ya utoaji wa matibabu ya kibingwa na bobezi itaenda haraka iwapo Madaktari hao wanapata wasaidizi wazuri katika kila kada kwenye maeneo ambayo watatoa huduma za afya hizo.
“Nichuku fulsa hii kuwaalika Wananchi wa Mkoa wa Singida kwa wenyeuhitaji wa huduma za kibingwa kujitokeza kwenye hospitali zote za Wilaya, Sitegemei Mwananchi yeyote kukosa huduma hizi za matibabu ya kibingwa na bobezi huduma ambazo huwa wanazifuata mbali na kwa gharama kubwa, hivyo lazima Wananchi wapewe taarifa ili wapate matibabu karibu na maeneo yao,” Amesisitiza Dkt. Fatuma Mganga.
Amewahakikishia ushirikiano Madaktari hao Bingwa na Bobezi katika kila jambo wanalofanya lengo ni kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanapata matibabu ya uhakikika kupitia madaktari hao wa Rais Samia.
Katibu Tawala pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa Watanzania wengi ambao baadhi yao wanashindwa kumudu gharama za kwenda kupata matibabu hayo kwenye Hospitali kubwa nchini na kwa sasa wanaipata karibu na maeneo yao.
Naye, Afisa Programu kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Uzazi, Mama na Mtoto Joachim Masunga, amesema mpango huo wa kutoa matibabu ya kibingwa na bobezi utafanyika nchi nzima nia ni kuona Mtanzania anapata huduma hizo karibu na maeneo yao na kuondoa tatizo la kufuata huduma hizo mbali na kwa gharama kubwa.
Masunga amesema kwa sasa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa Hospitali na Vituo vya afya pamoja na kupeleka vifaa vya kutosha vya afya lengo likiwa ni kusaidia Watanzania kupata huduma bora na za uhakika katika maeneo yao ikiwemo mpango wa kupeleka Madaktari bingwa na bobezi kwa kila Wilaya ili kusaidia wananchi kupata huduma hizo kwa njia rahisi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovick, akizungumza wakati wa kuwakaribisha Madaktari bingwa wa Rais Samia, katika Mkoa wa Singida.
Timu ya Uongozi wa Huduma za Afya Mkoa wa Singida (RHMT) wakati wa mapokezi wa Madaktari bingwa ndani ya ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.