• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MAGARI MAPYA KURAHISISHA UTENDAJI KAZI RUWASA, MAMLAKA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA SINGIDA

Posted on: November 6th, 2024

   Mkoa wa Singida umepokea  magari matano yenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni795  kwa matumizi katika Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida kwa ajili ya kusimamia shughuli za sekta ya maji.

Magari hayo yamekabidhiwa leo (Novemba 6, 2024) na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ni kwa ajili ya Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira  katika Wilaya za Singida mjini,Manyoni na Kiomboi, RUWASA Mkoa wa Singida na RUWASA Wilaya ya Iramba.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida,  Lucas Said, amesema magari hayo yametolewa ikiwa ni jitihada za kuhakikisha kwamba mamlaka hiyo zinasaidia kutatua kero za maji katika Mkoa wa Singida.

"Kama unavyofahamu tunaendelea kufanya kazi kuhakikisha kwamba tunafikia malengo ya kufikia asilimia 85 vijijini na mijini asilimia 95 ifikapo Disemba 2025,tunaendelea na jitihada ili kufikia malengo haya ambayo ni pamoja na kupata vitendea kazi ili viweze kusimamia miradi ipasavyo," amesema Said.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA),Sebastian Warioba, amesema baada ya kukabidhiwa magari hayo watahakikisha wanafikia malengo ya kufikisha maji kwa wananchi kama ambavyo imeainishwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Sisi watumishi wa sekta ya maji katika Mkoa wa Singida tunakuahidi tutaendelea kuchapa kazi kwa umoja,uadilifu na kujituma ili tuweze kufikia yale malengo ambayo yameainishwa kwenye ilani ya CCM,tunatoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa namna wanavyotujari na kutusimamia katika kuhakikisha tunamtua ndoo mama kichwani," amesema Warioba

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dendego,amesema kiwango cha upatikanaji wa maji kwa sasa kimefikia asilimia 68.2 vijijini na asilimia 86 mjini hivyo bado hakijafikia kwenye malengo ya ilani ya CCM.

"Kupewa magari haya tumeongezewa mwendo,tumeongezewa kasi na ari kuhakikisha ile miradi yetu tunayotekeleza sasa iweze kutekelezwa kwa kasi kubwa ili kufikia malengo yaliyopo kwenye ilani ya CCM kabla ya muda uliopagwa," amesema.

Dendego amesema Mkoa wa Singida umejiwekea malengo ikifika Juni 2025 malengo ya kufikia asilimia 85 kupeleka maji vijijini na asilimia 95 mjini yatakuwa yamefikiwa.

Amesema serikali chini ya Wizara ya Maji imekuwa ikiendesha kampeni ya kumtua ndoo mama kichwani  hivyo ili kufanikisha kampeni hiyo ni lazima kuwepo na vitendea kazi kama magari.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.