Watanzania wametakiwa kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa zoezi la Sensa ya majaribio kwa mwaka 2021 ya watu na makazi litakalofanyika katika vijiji 13 vya Tanzania bara katika mikoa ya Kigoma, Singida, Arusha, Dar es salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Njombe na Dodoma.
Akizungumza na wananchi hivi karibuni katika kitongoji cha kijaroda wilaya ya Mkalama mkoani Singida Kamisaa wa Sensa ambaye pia ni spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Semamba Makinda amesema sense hiyo ya majaribio itaanza tarehe 08 mpaka 19 mwezi huu hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kufanikisha zoezi hilo.
Aidha amesema zoezi la sensa ya majaribio kwa mwaka 2021 litatoa mwelekeo, fursa na changamoto katika kujipanga na sensa ya mwaka 2022.
“Tukifanya vizuri mwaka huu itakuwa ni dalili ya kufanya vizuri Zaidi mwaka kesho kwa sababu tutakuwa tumejifunza kutokana na changamoto za kipindi hiki” alisema Makinda.
Amesema sensa ya mwaka huu itakuwa ni tofauti na vipindi vingine ambayo ilikuwa inaishia katika ngazi ya wilaya na mkoa lakini kwa mwaka huu na mwaka kesho itakuwainafanyika hadi ngazi ya kitongoji.
Lengo la sensa hii ni kutaka kufahamu juu ya makazi majengo, anuani, idadi ya watoto, vijana na wazee ambao wapo ili waweze kuendana na bajeti ya Serikali. Alibainisha mama Makinda.
Aidha mama Makinda amesema sensa ni muhimu kwa taifa kwa sababu itasaidia kusukuma gurudumu la maendeo ya jamii, kusaidia kuratibu uwepo wa miundombinu ya shule, hospitali, barabara, makazi na hata mikopo kwa wanafunzi.
Akimalizia hotuba yake Kamisaa wa sensa Mama Makinda amewatoa hofu wananchi kwamba makarani watakaohusika katika zoezi hilo wamepata mafunzo ya kutosha na wamekula kiapo cha kutunza siri za watu wakati wa kuhesabu.
Naye mratibu wa sensa katika ngazi ya mkoa wa Singida Bw. Naeng’oya Kipuyo amesema maandalizi ya sensa mkoani hapo yamekamilika kwa kuwa tayari maeneo yameshatengwa na uhamasishaji umefanyika kwa kiasi kikubwa.
Amebainisha kwamba sensa ya majariibio kwa mkoa wa Singida itafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe nane (8) mpaka 10 ambapo wataalamu watangazia huduma za kijamii zinazopatikana eneo hilo.
Usiku wa tarehe 10 kumkia tarehe 11 itafanyika sense ya majaribio katika Kitogoji hicho kuhesabu watu waliolala katika nyumba zao zoezi litakalochukua siku tatu (3) mpaka tarehe 13 alibainisha bwana Kipuyo.
Amesema tarehe 14 mpaka 16 zoezi la sensa litaendelea katika Kitogoji hichio cha Kijaroda ambapo itafanyika sense ya majengo, wamiliki na huduma zinazofanyika katika nyumba hizo na mwisho ilatakuwa ni kuchukua anuani za makazi kwenye kila nyumba alimalizia bwana Kipuyo.
Mery christiani ni msichana mkazi wa Kitogoji hicho ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kuwasihi wananchi kutokuwa waoga na kuhakikisha wanajitokeza kuhesabiwa ikiwa ni pamoja na wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata mahitaji yao ya baadae .
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.