Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amewaongoza wakazi wa manispaa ya Singida katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya usafi katika sehemu mbalimbali za mji wa Singida.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi, Tarimo amesema Watanzania wakiwemo wa wilaya ya Singida wanapaswa kuuenzi Muungano huu kwa kushiriki kikamilifu maadhimisho yake.
Amesema bila Muungano huu ulioasisiwa na viongozi wetu hayati mwalimu Nyerere na mzee Abeid Karume, Tanzania ya leo isingekuwepo.
“Maadhimisho haya sasa yameboreshwa kwa maana yanaweza kufanyika kwa kufanya usafi kama tulivyofanya sisi leo au kwa mazoezi ya mwili. Niwasihi tu Watanzania wenzangu kuyathamini maadhimisho haya na kushiriki bila kukosa kila mwaka”, amesema.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Lyampembile amesema wananchi wa manispaa hiyo wamejitokeza kwa wingi na kushiriki vema kuadhimisha siku kuu ya Mungano.
“Ofisi yangu nayo imeshiriki watumishi wote ambao kwa siku ya leo afya zao ziko vizuri, wamejitokeza na kufanya usafi kama njia ya kuadhimisha siku kuu ya Muungano”, amesema Bravo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.