Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange, amesema ameridhishwa na ubunifu na maendeleo yaliyofikiwa katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kuwakwamua wananchi kiuchumi.
Naibu Waziri Dugange, ametoa kauli hiyo mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya Kimataifa yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesisitiza matumizi ya mashine na teknolojia za kisasa katika sekta hizo ikiwemo ya kilimo kama hatua ya kusaidia wakulima kuongeza maradufu uzalishaji na kupunguza gharama za uzalishaji na kuboresha kipato chao na cha Taifa kwa ujumla.
“Ukimwezesha Mkulima katika kilimo chenye tija unamwezesha kukua kiuchumi hivyo atapata mapato makubwa ambayo yatamsaidia kukuza uchumi wake na wa Taifa.” Amesisitiza Dkt Dugange.
Amesema maboresha katika sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi yatasaidia kwa kiasi kikubwa Halmashauri nchini kuongeza mapato yao kupitia sekta hizo iwapo tu maboresho yatafanyika kwa kiwango kinachotakiwa.
Naibu Waziri huyo amesisitiza Wadau mbalimbali walioshiriki kikamilifu hasa za zana za kilimo wahakikishe pamoja na kuuza zana zao wanakuwa na vipuli ili wananchi wasipate taabu ya vyombo vyao kusimama kufanya kazi kwa sababu ya kukosekana kwa vipuli hivyo.
Maonesho ya Nane Nane Kimataifa hukutanisha kwa pamoja Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Watafiti na watoa huduma mbalimbali ili kubadilishana maarifa na teknolojia mpya zinazolenga kuboresha sekta ya kilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, (mwenye kiremba) akimuongoza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange, kwenye maeneo ya maonesho ya Mifugo yaliyopo kwenye maonesho ya Nanenane jijini Dodoma.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange kuhusu kilimo cha Alizeti chenye tija zao linalolimwa kwa wingi mkoani Singida wakati Naibu waziri huyo alipotembelea sehemu ya Vipando vya Halmashauri ya Wilaya ya Singida leo (4 Agosti, 2024).
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.