"Michezo ni Afya"
Haya yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi wakati akizindua Mashindano ya Michezo mbalimbali kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Meimosi Kitaifa Leo tarehe 22 Aprili 2025 katika viwanja vya CCM Liti Mkoani Singida, Mashindano haya yalianza tarehe 16 Aprili na yatahitimishwa tarehe 30 Aprili.
" Michezo ni muhimu sana katika maisha yetu ili kujenga afya zetu lakini pia michezo inatufanya tuchangamke katika kufanya maamuzi na ni sehemu nzuri yetu wafanyakazi kujenga urafiki na kufahamiana"
Aidha, Katambi amesema serikali imetoa Fedha nyingi kuwekeza kwenye michezo kwasababu inaelewa na kutambua umuhimu wa michezo katika maisha yetu.
"Mhe. Rais ametoa Fedha nyingi kujenga viwanja kwenye mikoa mbalimbali ndani ya nchi yetu ikiwemo Arusha lakini pia uwanja wetu wa Mkapa umekarabatiwa vizuri kwasasa hiyo yote ni kuonesha umuhimu wa michezo hivyo tumuunge mkono Mama yetu ili tufike mbali"
Akizungumzia suala la Ushiriki wa Taasisi katika Mashindano haya kuelekea Maadhimisho ya Meimosi Naibu Waziri Katambi amefafanua kuwa Taasisi 44 zimeleta washiriki lakini zingine hazijaleta washiriki hii ni wazi kuwa hawaungi mkono juhudi za Mhe. Rais kwenye suala la Michezo na ikumbukwe kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ndio Muajiri namba Moja hivyo Wakuu wa Taasisi tujitahidi kuhakikisha tunaleta watumishi kushiriki Michezo hii"
Amebainisha kuwa Siku ya wafanyakazi Kitaifa ambayo itafanyika tarehe 01 Mei katika Mkoa wa Singida Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ndiye Mgeni Rasmi.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.