• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MATOKEO YA SENSA 2022 KUJA NA FURSA KABAMBE NCHINI

Posted on: January 28th, 2025

Mkuu  wa Mkoa wa Singida Mhe  Halima Dendego,ametoa wito kwa taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kutoa mafunzo kwa wanachama wa klabu za waandishi wa Habari katika Mikoa ili kuimarisha weledi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na usambazaji wa Habari kwa umma.

Mhe. Dendego ameyasema hayo leo Januari 28,2025  wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wanachama wa klabu za waandishi wa habari wa mikoa ya Dodoma na Singida kuhusu matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na tafiti nyingine za Takwimu yaliyoandaliwa na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

      “Kufanya hivyo kutaongeza kutangazwa kwa shughuli nyingi zaidi za maendeleo zinazofanyika mikoani zikiwemo zinazofanywa na wananchi wenyewe kama kilimo, ufugaji, uvuvi na nyinginezo nyingi ambazo zinagusa maisha ya siku ya wananchi sio tu wa vijijini bali hata wanaoishi mijini,”amesema Mhe.Dendego

Mhe. Dendego amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na Mpango Kabambe wa Pili wa Maendeleo ya Takwimu nchini (TSMP II). 

Aidha ameseema kuwa Mafunzo hayo yanakwenda sambamba lengo kuu la Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2022 ambalo ni kuongeza uelewa, uwazi na kupanua wigo wa matumizi ya Matokeo ya Sensa kwa Serikali, wananchi na wadau wote ili kupanga mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi, kijamii na mazingira. 

“Kamati za Sensa hazikuwa na uwezo wa kufika kila mahala lakini vyombo vya Habari vilifikisha ujumbe kila mahala bila kuwaacha wengine nyuma. Hivyo, sina budi kuvipongeza vyombo vyote vya Habari katika mikoa yetu ya Dodoma na Singida zikiwemo redio zetu za jamii kwa kujitoa kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa hadi tukafanikiwa kwa wananchi wote kuhesabiwa katika mikoa yetu” amesema Mhe Dendego 

Hata hivyo amefafanua  kuwa Lengo la Serikali ni kuona matokeo ya Sensa na ya tafiti nyingine za kitakwimu yanawafikia wadau wote hususani wananchi ili waweze kuyatumia katika shughuli zao binafsi na pia kuzitumia katika kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi ikiwemo kushiriki katika kufanya maamuzi ikiwemo kupanga, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali na wadau wengine wa maendeleo katika maeneo yao wanayoishi.

Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Tanzania Bara Mhe Anne Makinda, amesema kuwa kwa sasa serikali ipo katika Awamu ya Tatu na ya mwisho ya utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi. Awamu hiyo inajumuisha uchakataji, uchambuzi na uandishi wa ripoti pamoja na usambazaji, kufanya mafunzo na kuhamasisha matumizi ya matokeo ya Sensa.

Ameeleza kuwa awamu hiyo ni tofauti na tafiti nyingine za kitakwimu ambazo matokeo yake hutolewa mara moja kwa mkupuo, matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi hutolewa hatua kwa hatua kufuatana na Kalenda ya Utoaji wa Matokeo. Kama mlivyoona wakati wa zoezi la kuhesabu watu, Dodoso la Sensa lilikuwa na maswali karibu ya 100, hivyo taarifa zilizokusanywa zilikuwa nyingi kwa maana hiyo uchambuzi wake hufanyika hatua kwa hatua hadi kupata matokeo na kutoa ripoti kamili. Matokeo ya Ripoti hizi yakishazinduliwa rasmi husambazwa kwa njia mbalimbali ili kuwafikia wadau.

         Aidha amesema kuwa Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni mfufulizo wa mafunzo yanayoendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) ambayo yanafanyika kwa mujibu wa Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2022 na Lengo lake kuu ni kuvijengea uwezo waandishi katika kuchambua, kutafsiri na kutumia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na matokeo ya tafiti nyingine za kitakwimu zinazofanyika nchini ili viweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi zaidi.

Amesema mafunzo hayo yanaakisi msemo wa wahenga wa kupiga ndege wawili kwa jiwe moja. Kwa maana ya kutekeleza Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa na Mpango Kabambe wa Pili wa Maendeleo ya Takwimu nchini.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.