• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MBEGU ZA ALIZETI KUMALIZA TATIZO LA MAFUTA NCHINI

Posted on: February 19th, 2025

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amewataka wawekezaji wa Viwanda vya kuchakata mafuta ya kula mkoani Singida, kuhakikisha wanaimarisha uhusiano kati yao na wakulima, na kuingia mikataba yyenye tija kwa ajili ya kilimo, ili kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, kukidhi mahitaji ya mafuta ya kula nchini.

      Akizungumza baada ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa, cha kukamua mafuta ya alizeti, kinachomilikiwa na Kampuni ya Wild Flower Grain and Oil Mills, na kingine cha Mount Meru, Mkoani Singida, Naibu Waziri Kigahe amesema kuwa, ili kuongeza upatikanaji wa mbegu za mafuta ya alizeti, ni lazima mbinu mbalimbali ziweze kutumika, ikiwemo kuimarisha uhusiano na wakulima wote wa Mkoa wa Singida, na maeneo mengine nchini, yanayolima zao hilo.

Aidha Naibu Waziri amefafanua kuwa, licha kutumia njia hiyo, pia Wamiliki hao wa Viwanda watafanikiwa zaidi iwapo watasaidia na kuliwezesha kundi la vijana, kwa kuwapatia mashamba makubwa,  ili kujikita kwenye shughuli za kilimo cha alizeti, hivyo kuongeza upatikanaji wa zao hilona kuweza kukidhi mahitaji ya Viwanda.

Amesema Serikali imeboresha na kuimarisha upatikanaji wa mbegu Bora za alizeti, na kuwapatia wakulima mbolea kwa bei ya ruzuku, hivyo ni lazima pawepo na jitihada za makusudi, kuweza kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti na mengine kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Wananchi, hususani wakulima wa Mkoa wa Singida.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye  ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe.Godwin Gondwe, amesema kubwa msimu huu wa kilimo Mkoa wa Singida umepokea mbegu Bora ya zao la alizeti kutoka wakala wa Taifa mbegu za kilimo Tani 307, amabazo  zimesambazwa kwa wakulima, ili kuongeza upatikanaji wa zao la alizeti, msimu ujao.

"Mheshimiwa Naibu Waziri, tayari mbegu hizo zimewafikia wakulima mapema zaidi, ili hatimaye waweze kuotesha alizeti na kumaliza tatizo la mafuta ya kula hapa nchini, ambalo hulilazimu Taifa kutumia fedha nyingi, kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi,"alifafanua Mhe.Gondwe.

Kwa mujibu wa ofisi ya kilimo mkoa, mbegu hizo ni sehemu ya mahitaji ya Tani 2,000 zilizoombwa serikalini, kwa ajili ya kumudu kupandwa kwenye ekari zaidi ya milioni moja Mkoani Singida, lengo likiwa ni kuipunguzia mzigo Serikali kwa  kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

Naibu Waziri Kagahe, yupo kwenye ziara ya siku tatu mkoani Singida iliyoanza  Februari 18, kwa ajili ya kutembelea na kukagua Viwanda, Migodi na shughuli nyingine mbalimbali, zinazotekelezwa na Serikali, pia wawekezaji wa ndani na nje, ili kuchochea kasi ya ukuaji uchumi kwa jamii.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.