• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

*MHE.DENDEGO AZINDUA ZAHANATI NA KUZUNGUMZA NA WANUFAIKA WA TASAF

Posted on: November 10th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mhe Halima Dendego amewatembelea na kufanya mkutano na wanufaika wa mfuko wa kunusuru kaya masikini TASAF na kusikiliza kero na maoni mbali mbali waliyonayo  katika Kata ya Itigi Mjini,ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

Miongoni mwa malalamiko aliyopokea ni kuondolewa kwa idadi kubwa ya wazee katika unufaika wa TASAF walioomba serikali iwarudishe wapate huduma hiyo kwani ni ngumu kwa wao kuweza kumudu gharama za maisha na kujitegemea ili kujiingizia kipato kwani utendaji kazi wao umepungua sana na afya zao kutokua imara kutokana na umri kusogea.

Akijibu kero hiyo,Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa waratibu wa TASAF kuhakikisha wanafanyia kazi suala hilo kwa kuwarejesha wale wote wanaostahili katika mfuko huo na kuhakikisha malipo kwa wale ambao hawajapata fedha zao ndani ya muda wa miezi miwili kushughulikiwa kwa wakati.

Pia,alizindua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kashangu,Kata ya Idodyandole,zahanati  Iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na mwishowe kuungwa mkono na serikali na kukamilika kwa asilimia mia moja.

    Awali akisoma taarifa ya mradi,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kashangu,Twahil Amdan amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia watu zaidi ya 3200 kutoka katika maeneo ya Kashangu na maeneo ya jirani kupata huduma za afya bila kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.


Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua mradi huo,Mkuu wa Mkoa amewaagiza wahudumu wa afya kuzingatia huduma bora kwa kuhakikisha wazee,wajawazito na watoto wachanga chini ya miaka mitano wanapatiwa huduma bila malipo.Pia ameomba kuongezwa kwa wakunga wenye uzoefu wa muda mrefu kazini ili kuboresha na kutoa huduma bora na ya uhakika zaidi hasa katika masuala ya uzazi.

Pia ameahidi kutatuliwa kwa changamoto za uhaba wa maji ya kutosha katika eneo hilo,umeme,nyumba za watumishi na vyoo vya wafanyakazi kama miongozo inavyoelekeza.

Kupitia mradi huo,wananchi wataepukana na adha ya kusafir umbal mrefu kufuata matibabu,kusaidia wakina mama wajawazito kupata huduma wakati wa ujauzito na kujifungua,kurahisisha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango,chanjo na ufuatiliaji wa  karibu wa makuzi ya watoto chini ya umri wa miaka mitano.Pia utapunguza idadi ya wakina mama wanaojifungulia nyumbani au kwenda zahanati wakiwa katika hatua za mwisho za kujifungua.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.