Mwenge wa Uhuru 2021 mkoani Singida 24 Julai, 2021 ulikamilisha mbio zake katika Wilaya ya Manyoni kwa Miradi yote iliyokuwa inazinduliwa, inafanyiwa ufunguzi, inawekewa jiwe la msingi, inakaguliwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2021 yote imekubaliwa.
Julai 25, 2021 Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amekabidhi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati wa kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka, alisema Mkoa wa Singida unamuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii, kutunza amani na utulivu, umoja, mshikamano, mazingira na uhuru wetu hakika kazi iendelee.
Dkt. Binilith Mahenge alisema, Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Singida ulikimbizwa jumla ya Kilometa 642.3, ulipitia jumla ya miradi 55 inayohusu TEHAMA, Elimu, Afya, Mazingira, Maji, Biashara, Barabara na Program za Rushwa, Malaria, Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya, VVU/UKIMWI na Lishe.
Akifafanua zaidi alisema, Miradi 9 ilizinduliwa, miradi 2 ilifanyiwa ufunguzi, miradi 6 iliwekea jiwe la msingi, miradi 36 ilikaguliwa na miradi 2 ilitembelewa. Miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ilikuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 8,182,219,653.99
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Mwagisa wakati wa mapokezi ya Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Gery Muro alisema Mwenge huo utakimbizwa Wilayani hapo kwa muda wa masaa 24 ambapo utakagua miradi mitatu na Programu sita.
Aidha Mhe. Rahabu Mwagisa amesema Serikali ina lengo la kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma ya maji vijijini unafikia 85% ifikapo mwaka 2025 kwa hiyo ni jukumu la RUWASA na wadau wengine kushirikiana na Serikali kuhakikisha mpango huo unakamilika.
Hata hivyo Mhe Rahabu alibainisha kwamba lengo hilo la Serikali ili liweze kufanikiwa itaendelea kuwekeza katika ujenzi wa miradi mipya na ukarabati wa miradi ya zamani kwa kushirikiana na wananchi katika kuibua, kupanga, kutekeleza pamoja na usimamizi na uendeshaji wa miradi hiyo pindi inapokamilika.
Awali wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Ikungi Mhe. Rahabu alibainisha kwamba Mwenge wa Uhuru 2021 Wilayani Manyoni utakagua na kuzindua miradi Mitatu (3) na Programu sita (6) kama ifuatavyo.
Mapambano dhidi ya Malaria, Klabu ya wapinga Rushwa, Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Ujenzi Wa Mradi wa maji katika kijiji cha Kashangu kilichopo katika Wilaya ya Manyoni na Mradi wa Lishe.
Pia walizindua programua ya matumizi sahihi ya TEHAMA, Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja, Ujenzi wa Zahanati ya Masigati pamoja na Ushonaji ambapo yote ilizinduliwa.
Kwa upande mwingine LT. Josephine Paulo Mwambashi kiongozi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manyoni wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa Mradi wa maji wa kijiji cha Kashangu kilichopo katika Wilaya ya Manyoni amewataka kutunza miradi hiyo ili iwaletee mafanikio wananchi.
Hata hivyo ameipongea wakala wa maji na usafi wa mazingira vijiji RUWASA kwa kazi kubwa walioifanya ya kujenga na kusimamia vizuri miradi ya maji wilayani Manyoni na Singida kwa ujumla na kuwataka kujenga mazoea ya kuweka kumbukumbu vizuri wakati wa utekelezaji wa kazi zao.
Mungu Bariki Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 na Wakimbiza Mwenge Kitaifa
Mungu Ubariki Mkoa wa Singida,
Mungu Ibariki Tanzania
MWENGE WA UHURU HOYEEEEEE!!!!!!!!!
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.