Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida imepongezewa kwa kuongeza makusanyo ya mapato hadi kufikia asilimia 104 ikilinganishwa na Halmashauri nyingine.
Pongezi hizo zimetolewa leo (tarehe 26.06.2023) na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba, wakati wa kikao cha mapato kilichokutana katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo ambapo amesema mafanikio hayo yemetokana na ushirikiano mzuri kati ya Mkurugenzi, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya Moses Machali.
Amesema Halmashauri hiyo imekusanya mapato huru Bilioni 1.287 na mapato lindwa wakiwa wamekusanya Milioni 312.4 sawa na asilimia 104 wakati ikiwa imebaki siku tano kumalizika kwa mwaka wa fedha.
Amewataka Wakurugenzi wa Halamsahuri nyingine kuimarisha ushirikiano na kuepuka kuvutana baina ya viongozi jambo ambalo huweza kupunguza mapato na maendeleo kwa ujumla.
"Nasema nawapongeza sana Mkalama kwa kazi wanayofanya, ukiangalia makusanyo wamefikia asilia nzuri, ukiangalia miradi ya boost mingi imekamilika, na hii imetokana na ushirikiano wa viongozi" Serukamba
Hata hivyo ameendelea kuipongeza Manispaa ya Singida ambayo imeshika nafasi ya pili baada ya Mkalama ambapo makusanyo yamefikia asilimia 98 ikifuatiwa na Singida Dc yenye asilimia 91, Ikungi 89, Manyoni 82, Itigi asilimia 72 na ya mwisho ikiwa Iramba yenye asilimia 70.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali, akizungumza wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Singida
Sehemu ya Baddhi ya Wenyeviti wa Halmahsauri za Wilaya mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akielezea jambo wakati wa kikao hicho.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.