Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira SUWASA imetakiwa kuweka Mpango mkakati ya kuwa na mifumo ya ukusanyaji maji taka (sewage system) ambayo watayatibu na kuyarudisha tena kwenye matumizi ya kawaida ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba leo alipokuwa kwenye hafla ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya kutibu majitaka baina ya SUWASA na Mkandarasi M/S Perntels Company and Nangai Engineering and Contractors iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bonde la Kati.
RC Serukamba amesema ujenzi wa mabwawa hayo pamoja na kwamba yatawasaidia wananchi kuendesha shughuli za kilimo lakini bado yanaweza kusaidia upatikanaji wa maji ya uhakika endapo yatatibiwa na kurudi kwenye chanzo cha maji na kuendelea kutumiwa na jamii.
Aidha, amewataka SUWASA kuhakikisha wanaongeza wigo wa huduma za maji hasa maeneo ya pembezoni mwa miji ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji.
Amesema Mradi huo utagharimu kiasi cha Bilioni 1.73 na utatumia muda wa miezi 18 na utajengwa katika eneo la Manga katika Manispaa ya Singida.
Hata hivyo RC amewataka wananchi kuwapa ushirikiano mkubwa Wakala wa maji Safi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Singida SUWASA katika kipindi cha Ujenzi wa Mradi huo ambao utawasaidia kwa kiasi kikubwa hasa katika upatikanaji wa mazao ya bustani kutokana na uwepo wa maji ya umwagiliaji.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.