Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amesema wananchi wataendelea kuuenzi, kuheshimu na kutekeleza kwa vitendo ujumbe unao ambatana na mbio za mwenge wa uhuru ili kuchochea maendeleo ya wanasingida
Mhe. Dendego amesema hayo jana usiku katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati wa hafla ya mkesha wa mwenge wa uhuru ukitokea Jijini Mwanza kuelekea Mlima Kilimanjaro
" Mkoa unatambua kazi kubwa inayofanywa na mbio za mwenge wa uhuru ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na mshikamano sambamba na kuhamasisha maendeleo,toka ulipowashwa mwezi wa nne mwaka huu na kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani mwenge umeendelea kuwaimarisha watanzania "
Akiahidi kuendelea kusimamia yale yote yaliyokuwa yanahimizwa na ujumbe wa mbio za mwenge amesema wanasingida wana bahati kwa kuwa mwenge umelala mkoani humo wakati zoezi la wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa likiendelea.
Amempongeza Rais Dr Samia Suluhu Hasan kwa kuuteua Mkoa wa Singida kuwa sehemu ya kusindikiza Mwenge wa uhuru kuelekea mlima Kilimanjaro kwa kuwa hilo ni tukio linalobeba ujumbe mzito na kuweka kumbukumbu kubwa kwa watanzania.
Pia amewapongeza wanasingida kwa namna walivyojitoa hadi kupelekea Mkoa wa Singida kwa ujumla na halmashauri ya Ikungi kufanya vizuri katika mbio za mwenge kikanda kwa kushika nafasi ya kwanza na kuuheshimisha mkoa wa Singida kitaifa.
Ikiwa ni mara ya nne kwa Mwenge wa Uhuru kuplekwa mlima Kilimanjaro toka mwaka 1961,Mwaka huu Rais Samia Suluhu Hasan aliagiza mwenge wa uhuru upelekwe mlima Kilimajanro kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni pamoja,Mwenge wa uhuru kutimiza miaka 60 toka kuanza kwa mbio zake ,kusherekea miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Miaka 25 ya kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa .
Bendera ya Taifa na Mwenge wa Uhuru vitapandishwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na Kikosi maalumu cha Makamanda wa JWTZ kikiongozwa na Luten Kanali Halid Hamis Halid
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.