Miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 62.6 iliyojengwa katika halmashauri saba za zilizopo katika Mkoa wa Singida inatarajia kuzinduliwa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru 2025 ambao utakimbizwa kwa siku saba mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego, akitoa taarifa leo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu, Ismail Ally Ussi, baada ya kuupokea katika kijiji cha Sagara Halmashauri ya Wilaya ya Singida ukitokea Mkoa wa Manyara.
Amesema katika miradi hiyo mchango wa serikali kuu ni asilimia 92,asilimia 6.7 wahisani, halmashauri asilimia 1 na wananchi ni asilimia 0.2.
Mhe.Dendego amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Singida utakimbizwa jumla ya kilometa 842.6 katika halmashauri zote saba za mkoa huu na kwamba kila eneo wananchi wamejipanga kuupokea.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi Mkuu unaitarajia kufanyika Oktoba mwaka huu alisema mkoa umejipanga vizuri ambapo asilimia 99.6 ya wananchi wa Singida wamejiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.
Mhe.Dendego alisema katika kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya sita mkoa wa Singida umeweza kupokea Sh.trilioni 1.7 ambazo zimetumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji.
Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ndugu Ismail Ussi, ametoa wito kwa wananchi kuiishi kaulimbiu ya mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025 kwa kuhakikisha wanashiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.