Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Mhe. Elia Digha, ametoa wito kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, kuhakikisha bajeti zilizoombwa hazipunguzwi ili kuwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya halmashauri kufanyika kwa ufanisi.
“Hii bajeti inayoombwa, Mhe. Mkuu wa Wilaya, haipaswi kupunguzwa sana, si kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida pekee, bali pia kwa Manispaa ya Singida, ambao pia wamekuwa wahanga wa kupunguzwa kwa bajeti zinazopendekezwa,” alisema Mhe. Digha.
Mhe. Digha ameyasema hayo Januari 24, 2025 wakati akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichojadili utekelezaji wa mpango wa bajeti wa mwaka 2023-2024 na mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2025-2026.
Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Mwenge Sekondari, na kilihusisha Halmashauri mbili za Wilaya ya Singida, yaani Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Singida (Singida DC).
Mhe. Digha alisisitiza kuwa upunguzaji mkubwa wa bajeti unaweza kuathiri utekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi wa Wilaya ya Singida. Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya halmashauri na viongozi wa ngazi ya wilaya ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali za kifedha zinapatikana kwa wakati na zinalingana na mahitaji halisi ya maeneo husika.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.