• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

"Nataka taarifa ya kila mwezi kuhusu hali ya utoro shuleni" - RC Serukamba.

Posted on: April 27th, 2023

Walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani Singida wametakiwa kupeleka taarifa mkoani kila mwezi kuhusu hali ya utoro na mdondoko wa wanafunzi ili hatua madhubuti zichukuliwe kwa wazazi ikiwa ni hatua moja wapo ya kupambana na changamoto ya utoro.

Hayo yamesemwa leo tarehe 27.04.2023 na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Social Katoliki uliopo mjini hapo ambapo alikutana na wadau wa elimu kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu.

RC Serukamba amesema utoro na mdondoko wa wanafunzi kwa Mkoa wa Singida ni mkubwa  ambapo jumla ya wanafunzi 9,134 sawa na asilimia 11 ya wanafunzi walioandikishwa mwaka 2019 wakishindwa kufikia darasa la nne jambo ambalo amesema linaathiri ufaulu wa wanafunzi katika ufaulu na upimaji hasa wanapokuja kufanya mitihani.

Aidha amesema kwa sasa Serikali itahakikisha inawachukulia hatua kali wazazi watakao bainika kuwaficha watoto wasiende shuleni lengo likiwa ni kuinua kiwango cha elimu mkoani hapa.

Aidha RC amebainisha kwamba mbali ya utoro wa wanafunzi changamoto nyingine inayosabisha kurudi nyuma kwa elimu ni ukosefu wa chakula shuleni ambapo shule 479 sawa na asilimia 78 ya shule za msingi hazipati chakula ikiwa ni pamoja na sekondari  53 sawa na asilimia 40.85 jambo ambako linachangia kuzorotesha elimu.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amesema jumla ya wanafunzi 34,029 sawa na asilimia 10.18 hawamudu Stadi za KKK ambapo amewataka Wakuu wa shule kusimamia kikamifu kuhakikisha hali hiyo inakwisha.

RAS amesisitiza walimu kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo matumizi ya vijiti na visoda kama nyenzo itakayomsaidia mtoto kujua kuhesabu kwa mbinu hizo ndizo zikitumika awali na zilionesha mafanikio.

Hata hivyo amewaomba wazazi kusaidia upatikanaji wa chakula cha wanafunzi shuleni hasa kipindi hiki cha mavuno kwa sababu Serikali hazitaweza kutoa kwa kila mtoto ili kuboresha elimu.

Dkt. Mganga amefafanua kwamba Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya shule ikiwepo ujenzi wa madarasa vyoo na kuongeza walimu hivyo kutoa wito kila mdau kuhakikisha anatekeleza wajibu wake.

Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza wakati wa kongamano hilo.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.