MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesema pato la Mkoa huo (GDP) limeongezeka kutoka Sh. Trilioni 2.8 mwaka 2020 hadi kufikia Sh. Trilioni 3 kwa mwaka 2021.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha miezi sita leo (Februari 19) kwenye kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, amesema wastani wa pato la kila mtu kwa mkoa huu limeongezeka kutoka Sh.1,651,785 mwaka 2020 na kufikia Sh.1,721,195 mwaka 2021.
Serukamba amesema kumekuwa na ongezeko la mpango wa bajeti ya Mkoa wa Singida kutoka Sh.199,170,767,000 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia Sh.239,808,971,000 mwaka 2022/2023.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata ambaye aliongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa kukagua miradi inayotekelezwa mkoani Singida, amesema CCM imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo na kwamba hiyo imetokana na ushirikiano mzuri kati ya chama na viongozi wa Serikali.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata akitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali Mkoa wa Singida kutokana na utekelezaji mzuri wa Miradi ya Maendeleo mkoani hapo wakati wa kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Disemba 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Februari 19, 2023.Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akitoa taarifa kwa viongozi wa Serikali Mkoa wa Singida na wajumbe wa kikao cha Halmashauri kuu CCM Mkoa kutokana na ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Disemba 2022 wakati wa kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Februari 19, 2023.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza jambo wakati wa kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Februari 19, 2023.
Kikao kikiendelea
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.