Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amezihimiza mamlaka za maji na mabondeya maji kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kujiendesha vyenyewe bila kutegemea serikali kuu.
ProfesaMkumbo ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka ya majiSingida (SUWASA), Bonde la maji kanda ya kati na maabara, mjini hapa mjini .
AmesemaSerikali haina fedha za kukidhi mahitaji yote ya mamlaka za maji na mabondenchini hivyo ni vema vikaweka mikakati ya kujitengemea kimapato.
“Duniani kotehata Marekani haitoi fedha kwa taasisi kama hizi zenu. Tumieni kalamu na akilizenu kwa ajili ya kuandika maandiko yatakayowasaidia kupata fedha zakujiendesha bila kutegemea serikali au wafadhili”, amesisitiza.
Akisisitizazaidi, kwa kusema umefika wakati sasa mamlaka na mabonde ya maji, zifikiriekuwekeza na kujiwekea mipango thabiti ya kuongeza mapato yao.
Aidha, KatibuMkuu huyo amewataka watumishi wa SUWASA, kutoa huduma bora itakayovutiawananchi wengi zaidi kupata huduma ya maji katika mamlaka hiyo.
“Watejawa maji ndio wanaowalipa ninyi mishahara na stahiki zingine. SUWASA ikiwana wateja wachache kwa vyo vyote uendeshaji wake utakuwa mgumu na hivyo hivyoupatikanaji wa mishahara yenu nao utakuwa mgumu”, amesema Profesa Mkumbo.
Ameongezakuwa SUWASA na mamlaka nyingine za maji nchini ni lazima ziwe na mkakati wakupanua wigo wa wateja.
“Utamaduni wakutoa huduma bora unamfurahisha mteja na atapenda kuendelea kuwa mteja waSUWASA wakati wote. Pia itawavutia watu wengi kukimbilia huduma borazinazotolewa na SUWASA”,alisema.
Katikahatua nyingine, Profesa Mkumbo ametumia nafasi hiyo kusisitiza utaratibu wa kulipiakwanza (pree paid) maji kabla ya kupata huduma ya maji.
Amesema utaratibu huo utasaidia kuepukana na wateja wakorofi ambao huzalishamadeni sugu na kusababisha mamlaka kushindwa kutoa huduma zinazokidhi mahitajiya wateja.
“Kupitiautaratibu huu mteja husika ni lazima ajue matumizi yake ya maji kwa kipindi chamwezi. Baada ya hapo analipia kiwango hicho cha maji halafu ndipo apewe maji yakiwango alicholipia”, amesema katibu mkuu huyo.
Awali Afisa Maji bonde la kati Benard Chikarabhani amesema wameanza utekelezaji waujenzi wa bwawa la Farkwa kwa lengo la kuongeza usambazaji wa maji katika mjiwa Dodoma, Bahi, Chamwino na halmashauri ya wilaya Chemba.
“Bwawa hilolinatarajiwa kuwa na kiasi cha maji cha mita za ujazo 470,000,000 na litachukuaeneo la kilometa za mraba 68 pia bwawa litatumika kuboresha kilimo chaumwangiliaji katika mradi wa umwangilaji Bahi”, amesema Chikarabhani.
Wakatihuo huo, Chikarabhani amesema bodi ya maji bonde la kati inatarajia kutumiazaidi ya shilingi bilioni 2.4 kugharamia ujenzi wa ofisi makao makuu mjinihapa.
“Fedha hizozitagharamia pia ukarabati wa ofisi na maabara katika ofisi ndogo ya bodizilizopo mkoani Shinyanga. Vile vile ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumijai majiya Mto wa Mbu”, amesema afisa huyo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.