Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi yake ya kutoa Sh.Milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Taqwa ambayo aliitoa kupitia kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi.
Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Omari Muna, alikabidhi hundi ya malipo ya fedha hizo jana kwa Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro hafla iliyoshudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego na waumini, iliyofanyika Januari 10,2025.
Hapi akizungumza kwa njia ya simu alisema Rais amekuwa akisaidia mara kwa mara ujenzi wa misikiti na makanisa kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa Watanzania hivyo wananchi warudishe shukrani kwake kwa kuendelea kumuombea.
Alisema fedha hizo zitumike vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa ili rais na wadau wengine wanapoona kazi imefanyika vizuri waone umuhimu wa kuendelea kutoa zaidi kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo.
" Niwaombe tuendelee kumuombea dua na afya njema Rais wetu kwani mambo anayoyafanya ni kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa Watanzania na ninampongeza Sheikh wa mkoa kwa kuwashirikisha waumini katika suala hili la ujenzi wa msikiti,” alisema.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Singida, Nassoro, alimshukru Rais Dk.Samia kwa mchango wake huo na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono rais kutokana na mambo makubwa ya maendeleo anayoyafanya katika nchi yetu.
Sheikh Nassoro alisema katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 wananchi waendelea kudumisha amani na upendo kama ilivyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego, alimshukuru Mhe. Rais Dk. Samia kwa mchango huo wa ujenzi wa msikiti ambapo aliunga mkono kwa kuchangia Shilingi Milioni 5.
“Tunawashukuru wale wote walioguswa katika kuchangia ujenzi wa Msikiti huu ambapo zimefikia jumla Shilingi milioni 176 , kila mmoja aliyeguswa apate baraka za Mungu,” alisema Mhe.Dendego
Hata hivyo, alisema malengo ya ujenzi huu bado hayajafikiwa hivyo Waislam na wadau wengine waendelee kuunga mkono kwa kuchangia pesa hasa ikizingatia msikiti huo upo katikati ya mji wa Singida, hivyo ni lazima uonekane wa kisasa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.