Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni kama hatua ya kukomesha tatizo hilo ambayo limeonekana kuwa ni kero kubwa katika maendeleo ya sekta elimu mkoani Singida.
Dendego ametoa kauli hiyo (tarehe 20 Aprili, 2024) katika ziara yake ya kikazi ya Siku Mbili katika Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakati anakagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu na kuzungumza na Jumuiya ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kitaraka wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Singida amesema ili kukomesha tatizo hilo yeye ataanza kukamata kwanza msichana aliyepata mimba na baadaye mvulana ambaye atakuwa mtuhumiwa namba mbili kama hatua ya kukomesha vitendo vya mimba kwa wanafunzi.
“Nikikuta msichana umepata mimba wewe utakuwa mshtakiwa namba Moja na wewe ndio utakayeenda jela bila huruma na tumbo lako utajifungulia huko huko kwa sababu mna tabia ya ukipata mimba tunaenda kukimbizana na mtoto wa kiume si sawa wote mlishirikiana kwa hiyo yeye atakuwa mstakiwa namba mbili na msichana atakuwa mstakiwa namba Moja,” Amesisitiza Halima Dendego.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya Mwalimu inayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kitaraka Halmashauri ya Itigi.
Naye, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwa mfano kwa wazazi na jamii nzima na kuachana na mambo yanaenda kinyume cha maadili ya Kitanzania.
Fatuma Mganga, amesema kuwa kama wanafunzi watasoma kwa bidii hadi Vyuo Vikuu watakuwa na faida kubwa sio tu kwa familia zao bali kwa jamii nzima na Taifa kwa ujumla kwa sababu Serikali imeboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kitaraka iliyopo Halmashauri ya Itigi mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya Mwalimu.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya Mwalimu inayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kitaraka Halmashauri ya Itigi.
======
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.