Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, amewaagiza Waaajiri wote mkoani humo kuhakikisha wanaruhusu Mabaraza ya Wafanyakazi kufanyika sehemu za kazi ili kujua changamoto na matatizo yanayowakabili wafanyakazi kwa nia ya kutafutia ufumbuzi haraka matatizo yanayowakabili nia ikiwa ni kuongeza ari na ufanisi sehemu za kazi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Kimkoa wilayani Ikungi Mei 1, 2024 katika viwanja vya standi ya zamani.
RC Dendego, amesema Mabaraza ya wafanyakazi yanafaida kubwa kwa sababu yanarahisisha kujua changamoto za Wafanyakazi zinazoweza kusababisha kuzorota kwa ufanisi wa kazi hivyo changamoto zikitafutiwa majawabu mapema zisaidia wafanyakazi kuongeza bidii na ufanisi kazini.
“Mimi sio Muumini wa Watu wanaovunja Sheria hivyo Waajiri Wakatakao kaidi Maagizo yangu nitashughulika nao” Amesisitiza RC. Halima Dendego.
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Singida ameonya kuhusu Waajiri ambao hawaruhusu wafanyakazi wao kuanzisha au kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi na kusititiza kuwa jambo hilo ni kinyume cha taratibu na lazima likomeshwe haraka.
Kuhusu, Madeni ya Wafayakazi Mkoani Singida, Dendego amesema mkoa huo unaendelea na mchakato wa kulipa madeni ya wafanyakazi na kusema kuwa Wafanyakazi wa mkoa huo walikuwa wanaidai Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni 1.9 na mpaka sasa Serikali imewalipa Wafanyakazi zaidi ya shilingi Milioni 700.
Amesema dhamira ya Serikali ya kulipa madeni ipo pale pale kinachotakiwa ni uvumilifu tu.
Halima Dendego amewataka Waajiri wahakikishe wanaacha tabia ya kuzalisha madeni mapya ikiwemo kuhamisha watumishi bila stahiki zao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA) mkoa wa Singida Bi. Agnes Lucas ameishukuru Serikali kwa kuendelea kulipa madeni ya Wafanyakazi, upandishaji wa madaraja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia vitendea kazi vya kisasa hali ambayo imesaidia kuongeza ari na uwajibikaji Sehemu za kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa huo Dkt. Fatuma Mganga kwenye hafla ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa Wilayani Ikungi
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.