Watendaji wa Vijiji na Kitongoji kwa kushirikiana na madiwani pamoja na wananchi wa Mkoa wa Singida wametakiwa kushirikiana ili kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa maeneo yowazunguka.
Akiongea wakati wa ziara yake iliyofanyika leo katika Kata ya Rungwa Halmashauri ya Itigi, Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amesema Serikali imetoa fedha nyingi mkoani hapo ili kutekeleza miradi ya ujenzi wa Mashule, barabara na Vituo vya Afya ambapo maeneo mengi wananchi wamekuwa wakishiriki kikamilifu shughuli mbalimbali katika miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.
RC Mahenge ametoa wito huo alipotembelea miradi ya ujenzi wa vituo shikizi (shule shikizi) za sekondari na msingi zikihusisha kituo cha Kudema kilichopo Kata ya Rungwa, kituo shikizi cha Itaga kilichopo kitogoji cha Mkola na Ngirimalale kilichopo kata ya Mwamagembe wilayani Itigi.
Aidha ametumia ziara hiyo kuhamasisha wananchi kushiriki utekelezaji wa kazi za miradi ambapo RC huyo amejitolea kujenda matundu manne (4) katika vituo viwili vya Kudema na Itaga ambavyo vinagharimu jumla ya Sh. Milioni nne.
Hata hivyo RC ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha hizo ambazo zimesaidia kuimarisha na kuongeza miundombinu ya elimu wilayani Itigi eneo ambalo shule zilikuwa mbalimbali na makazi ya watu hivyo kupunguza tatizo la kutembea umbali mrefu .
Naye Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Itigi John Mgalula amemueleza Mkuu wa Mkoa kwamba vituo hivyo shikizi ni muhimu sana kwa kuwa kituo kimoja kina watoto wapatao 350 hivyo vitawasadia wote wanaokaa mbali na shule na wenye umri mdogo.
Mkurugenzi akamuomba RC kwamba baadhi ya vituo hivyo kubadilishwa na kuwa shule kwa kuwa fedha zilizotolewa na Serikali zimekuwa msaada mkubwa sana katika kuimarisha miundombinu ya vituo hivyo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.