Wananchi wa Halmashauri ya Itigi katika Kata ya Rungwa wametakiwa kutunza Mazingira kwa kupanda miti ambayo itasaidia kupunguza uharibifu wa Mazingira na kulinda barabara ambayo inaendelea kutengenezwa.
Kulingana na Mazingira ya Rungwa Barabara zimekuwa zikiharibika kutokana na kukatwa miti na kusababisha mmomonyoko wa ardhi na maji kuhama katika mikondo yake.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ameyasema hayo tarehe 9.11.2021 alipofanya ziara ya kukagua barabara ya Rungwa, Itigi na Mkiwa yenye urefu wa Kilomita zaidi ya 200.
Akiongea akiwa katika daraja la Rungwa ambalo ni mpaka kati ya Singida na Mbeya Mkuu wa Mkoa amesema barabara hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi kwa kuwa inaunganisha mikoa mitatu ya Mbeya, Singida na Tabora ambapo itasaidia kuongeza mzunguko wa kibiashara katika mikoa hiyo.
Amesema kukamilika kwa Barabara hiyo kunatoa fursa ya kuunganisha Tanzania, Zambia na Malawi ambazo zote zinatumia nchi za maziwa makuu kufanya Biashara ikiwa ni pamoja na nchi nyingine za Afrika mashariki ambapo zitaongeza muingiliano wa shughuli za kibinamu.
Amesema utunzaji wa Mazingira utasaidia kulinda kingo za mito zisiweze kuvunja barabara ambapo amesema kwa kutunza Mazingira kutasaida kupata fedha za kigeni kwa kupunguza hewa ya ukaa Nchini.
Akimnukuu Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu, MKuu wa Mkoa wa Singida amesema Tanzania imeingia makubaliano ya kutunza na kuhifadhia Mazingira ambapo mikataba mbalimbali imesainiwa hivyo ni jukumu la kila mtanzania kutunza na kuhifadhia mazingira.
Amewakumbusha wananchi kutuza Mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yote ili kuzuia uchepushaji wa maji ya mvua ambayo yamekuwa yakiharibu Barabara.
Aidha ametoa wito kwa wakandarasi hao kuhakikisha kila mmoja anamaliza kazi yake kabla ya kuingia katika kipindi cha mvua nyingi ili kutozuia shughuli mbalimbali za wafanyabiashara na wasafiri.
Awali akieleza Hali ya mradi huo Mhandisi Matare Masige, Meneja wa TANROAD Mkoa wa Singida amesema Mradi unagharimu kiasi cha sh.Bilion 1.5 na unatekelezwa na wakandarasi watatu na utawasaidia wananchi wa mikoa ya Sikonge, Manyoni na Mbeya pamoja na mikoa ya jirani.
Amesema barabara hiyo imegawanywa katika vipande vitatu kulingana na idadi ya wakandarasi ambao ni M/s Jam Engineers ambayo italipwa kiasi cha sh.milioni 348.3 na M/s Madata In.Ltd ambayo imeingia mkataba wa Milioni 592.7 wakati Kampuni ya M/S JP Treders Ltd imeingia mkataba wa Sh. Milioni 567.93
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba wakati wa ziara ya ukaguzi wa barabara ya Rungwa - Itigi iliyofanyika hivi karibuni
Meneja wa TANROAD Mkoa wa Singida Mhandisi Matare Masige (kushoto) akielezea jambo wakati wa ziara.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.