Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameiagiza halmashauri ya Manispaa ya Singida kusimamia upatikanaji wa mizinga hamsini ya nyuki kwa ajili ya timu ya mpira wa Miguu ya Misuna Stand kwakuwa imekua ni timu yenye lengo la kuwa kituo cha mafunzo na marekebisho ya tabia.
Dokta Nchimbi ametoa agizo hilo mapema leo asubuhi alipokutana na wananchama wa klabu hiyo ambapo amewaomba radhi kwakuwa Mkoa, wilaya na Halmashauri ya manispaa imekuwa haitoi ushirikiano wa kutosha kwa timu hiyo.
Amesema timu hiyo ambayo imeundwa na umoja wa Mawakala wa Mabasi Singida, imekuwa mstari wa mbele wa kubadilisha tabia mbaya kuwa njema hasa kutokana na mazingira ya stendi nyingi nchini kutawaliwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.
Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa sasa serikali ya Mkoa, wilaya na halmashauri imewatambua na kwa kuthibisha hilo yeye kama mkuu wa mkoa amejiunga ramsi kama mwananchama wa timu hiyo ya mpira wa miguu na kutoa michango ya miezi mitatu ambapo kila siku mwanachama anatakiwa kuchangia shilingi miatano.
“Nimetoa ada ya uanachama kuonyesha kuwa tupo pamoja na tutashirikiana kuhakikisha timu yetu ya Misuna Stand inapanda daraja, kwa sasa nawaomba wanachama wote tushirikiane katika kuiboresha timu yetu”, amesisitiza.
Dkt. Nchimbi amesema lengo la Mkoa ni kuwa na timu mbili za mpira wa miguu ambazo zinashiriki ligi kuu na kwakuwa tayari uwanja wa nyumbani wa Namfua Stadium uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji huku akiwahakikishia mashabiki wa Singida United kuwa wataishuhudia timu yao ikicheza nyumbani.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo ambaye ameteuliwa kuwa Mlezi wa Timu hiyo amesema stendi zimekuwa ni mahala pa wizi, uvutaji wa madawa ya kulevya na vitendo viovu lakini jitihada za Misuna Stand FC zitabadilisha tabia hizo na kuwa njema.
Tarimo amesema wanachama watakuwa wachapakazi kwakuwa kila siku wanatakiwa kulipa kiasi cha shilingi miatano lakini pia wamejipanga kuhakikisha wanaelimishana juu ya madawa ya kulevya jambo ambalo litaufanya Mkoa na Mji wa Singida kuwa wa Amani sana.
Ameongeza kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji waq agizo la Mkuu wa Mkoa La kuipatia timu hiyo Mizinga hamsini pamoja na kuhakikisha halmashauri inatoa eneo la utundikaji wa miznga hiyo pamoja na kuitunza.
Naye Mwenyekiti wa tawi la Misuna stand FC Yahya Said Kisiu amesema wanachama wa timu hiyo wamepata faraja kubwa sana kwa kutembelewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na kuwapatia mizinga hamsini.
Kisiu ameongeza kuwa timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014 ilifanikiwa kufika ligi daraja la pili lakini kwa sasa imeshuka tena daraja huku akisisitiza kuwa ari mpya waliopatiwa mkuu wa Mkoa itawezesha timu hiyo kupanda tena daraja.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.