Wafanyabiashara Mkoani Singida wamesisitizwa kutoa na kudai risiti halali wakati wa mauziano baina yao ili kuongeza mapato ya Serikali huku TRA wakitakiwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa ulipaji kodi kwa hiari.
Akiongea jana tarehe 27.06.2023 wakati wa jukwaa la wadau wa Kodi Mkoani Singida lilofanyika katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya KBH iliyopo mjini Singida Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, ameeleza kwamba wafanyabiashara wanatakiwa kuitendea haki nchi kwa kulipa kodi stahiki na kuhakikisha wanatoa risiti kulingana na kiasi cha fedha alichotoa mteja.
Aidha amesema inashangaza kuona Wafanyabiashara wanakaa kujadili namna ya kukwepa Kodi huku wengine wakiweka visingizio kwamba Kodi zinazotozwa sio rafiki kwa mfanya biashara.
Hata hivyo RC Serukamba amesema kuna haja ya kurekebisha sheria ya Kodi inayomtaka mfanya biashara mwenye mtaji usiozidi Tsh.Milioni Nne kwa kuwa wapo Wafanyabiashara ambao hugawanya mtaji makusudi na kuwa na maduka zaidi ya moja lengo likiwa kukwepa Kodi.
RC ameagiza TRA kuendelea kutoa elimu ya Kodi kwa wananchi na kuwafahamisha wananchi kwamba Serikali imeweka viwango vikubwa vya faini kwa lengo la kukomesha ukwepaji wa Kodi na sio sababu ya kuongeza mapato.
Maelezo hayo yalitokana na moja ya mjumbe aliyelalamika kwamba faini ya Tsh Milioni Nne kwa anayekamatwa kwa kuuza bila kutoa risiti ipunguzwe kwa kuwa inaruhusu mazungumzo yenye sura ya rushwa baina ya TRA na wafanya biashara.
Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa Singida Issa Nassoro, amewataka wananchi kulipa kodi kwakuwa kwa upande wa dini yao yeye aliifananisha na zaka hivyo kuomba timu ya TRA Mkoani hapo kuendelea kutoa elimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida akizungumza wakati wa jukwaa la wadau wa Kodi Mkoani Singida
Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida Hasan Ramadhani Mzee, akizungumza wakati wa jukwaa la wadau wa Kodi Mkoani Singida
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.