Wakulima wa bustani katika Kata ya Nkalakala Wilayani Mkalama wameiomba Serikali iwasaidie upatikaji wa mbolea za kupandia na kukuzia ziweze kupatikana katika kipindo chote cha mwaka kwa kuwa kilimo chao hakina msimu maalumu.
Kauli hiyo imetolewa leo wakati Mkuu wa Mkoa huo, Peter Serukamba akisikiliza na kutatua kero kwa wananchi wote wa kata ya Nkalakala ambapo wakulima wa bustani wakilalamikia kukosekana mbolea hizo katika vipindi vya nje ya msimu wa kilimo cha mahindi na alizeti.
Wakulima hao wamedai kwamba kilimo chao hakina msimu hivyo wanapata changamoto kubwa ya kufuata mbolea Mkoani Arusha au Manyara hivyo kuomba Serikali ifanye mpango zipatikane katika maduka ya pembejeo wakati wote zinapohitajika ili ziwasaidie kuinua kilimo chao.
Akijibu hoja za wakulima hao Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba amesema Serikali imepokea maombi hayo na atafanya Mawasiano na Waziri wa Kilimo ili kupata Wakala ambaye atasabaza mbolea hizo katika kata zote .
Amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Mkalama kwa namna walivyojitoa kulima mazao yote ya chakula na biashara ambapo ameahidi kuwaeleza wahusika kuhusu changamoto zinazosabisha kushuka kwa soko hasa zao la alizeti na huku akitaja mafuta kutoka nje ya nchi ambayo hayana kodi kwamba yanachangia kuangusha soko hilo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.