MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesisitiza kuwa uamuzi alioutoa wa kutaka malori inapofika saa 2:00 usiku yapelekwe kuegesha kwa ajili ya kulala katika stendi ya Manyoni utabaki kama ulivyo kwa kuwa umesaidia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kupata mapato kutokana na ushuru wa magari hayo.
Ametoa msisitizo huo wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika hivi karibuni katika kitongoji cha Majengo Kata ya Manyoni ambao wananchi walimweleza kuwa uamuzi wa kupiga marufuku malori yasiwe yanaegeshwa pembezoni mwa barabara kumeathiri biashara zao.
Mhe. Serukamba alisema kuanzia asubuhi hadi saa 2:00 usiku ni ruhusa malori kupaki pembenezoni mwa barabara lakini baada ya muda huo yapelekwe stendi ambako yatalazimika kulipa ushuru wa stendi wa Sh. 3,000 kwa kila gari fedha ambazo zinaingia halmashauri na kusaidia kwa ajili ya maendeleo.
Alisema kimsingi wanaolalamikia suala hilo ni wale ambao walikuwa wakinufaika binafsi na malori yanapopaki pembezoni mwa barabara ambapo fedha za ushuru zilizokuwa zinatolewa na wenye magari zilikuwa zikiwanufaisha wao binafsi na hivyo halmashauri kukosa mapato.
Serukamba alisema kabla ya kuweka utaratibu huo miezi miwili iliyopita, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ilikuwa ikipata ushuru Shilingi Milioni mbili tu kwa mwezi kutokana na ushuru wa malori kupaki pembezoni mwa barabara lakini hivi sasa kwa mwezi zinakusanywa zaidi ya Shilingi milioni 4 kwa mwezi ambazo zinaingia moja kwa moja halmashauri.
Aidha, Mkuu wa Mkoa aliendelea kuwakumbusha wafanyabiashara wote mkoani Singida kuhakikisha wanalipa kodi ili Serikali iweze kupata mapato ambayo yatatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Manyoni JIMSON PETER MHAGAMA akizungumza wakati wa mkutano huo
Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Manyoni akizungumza wakati wa mkutano huo
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.