Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba tarehe 25/04/02023 amewaagiza Wakala wa Barabara TANROAD kupanda miti, kuweka vizuizi katika mifereji inayozunguka daraja hilo la chini ili kusaidia kutunza Mazingira na kuepusha ajali kwa wakazi waliopo jirani na mifereji hiyo.
Kauli hiyo ameisema wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa kivuko cha watembea kwa miguu kilichojengwa katika Manispaa ya Singida katika eneo la Kibaoni ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano ambapo kwa Mkoa wa Singida kilele kitafanyika shule ya msingi Minga.
RC Serukamba ameeleza kwamba kivuko hicho ni muhimu kwakuwa litanusuru watembea kwa miguu wakiwemo wanafunzi ambapo ameeleza kwamba eneo husika ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
Hata hivyo RC Serukamba ameukataa muongozo wa Wakala hao ambao ulikuwa kuwaruhusu wananchi kufanya biashara katika eneo hilo akieleza kwamba eneo libaki kuwa kivuko na biashara zikafanyike maeneo mengine.
Aidha, ametumia wakati huo kuongea na wanafunzi wa shule ya msingi Kibaoni kuwaeleza maana na umuhimu wa Muungano katika kuleta amani na kuimarisha usalama huku akiwasisitiza wanafunzi kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu ili kuongeza ujuzi.
Akiwa katika eneo la daraja amewataka wananchi na wanafunzi kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yao isiyopungua minne kwa kila kaya ili kutunza mazingira kwa faida ya watu wote.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANROAD Mkoa wa Singida amesema daraja linafahamika kwa jina la (underpass) katika barabara ya Kintinku - Singida - Malendi ambalo limegharimu milioni 427.8
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.