Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba, amekemea utaratibu wa kukusanya fedha bila kuzipeleka Benki jambo ambalo ameeleza kwamba linashusha asilimia za ukusanyaji hasa katika mfumo mpya wa ukusanyaji mapato Serikalini (TAUSI).
Akiongea leo (tarehe 26.06.2023) wakati wa kikao cha kujadili hali ya mapato mkoani hapo ambapo amesema kwamba walikubaliana na Wakurugenzi kwamba fedha itakayokusanywa ipelekwe Benki lakini anashangaa jambo hilo likiendelea.
Mkuu wa MKoa wa Singida akisoma taarifa ya Halmashauri ambazo hazijapepelea fedha Benki.
Amesema Halmashauri ya Singida imekusanya Tsh. Milioni 21, Ikungi Milioni 17, Iramba Milioni 17, Singida Manispaa Milioni 15, Mkalama Milioni 4, Itigi Milioni 3.1 na Manyoni Milioni 1.1 ambazo zote hazijapelekwa Benki.
"Watunza hazina wa Halmashauri msikubali fedha iliyokusanywa ikae bila kuwekwa benki ikasomeka kwenye mifumo na hili linaturudisha nyuma" RC Serukamba.
Hata hivyo ameagiza kwa muda uliobaki kila Halmashauri iwe imekusanya zaidi ya asilimia 98 ambapo itakuwa imeuweka mkoa katika nafasi nzuri ya kiushindani.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, akizungumza wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Singida wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisisitiza jambo wakati wa kikao.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.