• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC SINGIDA AAGIZA KUKAMILISHWA KWA MIRADI YOTE YA MAENDELEO HADI KUFIKIA MWISHONI MWA MWEZI HUU.

Posted on: August 14th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewaagiza Watendaji katika Halmashauri Saba za mkoa huo kuhakikisha wanakamilisha utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo hadi kufikia mwisho mwa mwezi huu.

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ametoa agizo hilo (14 Agosti, 2024) katika majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Manispaa ya Singida.

Dendego amesisitiza kuwa miradi yote iliyoanza kutekelezwa katika kipindi cha miaka Mitatu nyuma lazima ikamilike ili wananchi waanze kupata huduma mbalimbali za kijamii kwa muda muafaka.

“Lengo la miradi hii sio kuona majengo bali ni kutoa huduma inayotakiwa lazima majengo yakamilike kwa wakati na kwenye matatizo Viongozi wakae na kutatua changamoto hiyo ili miradi isikwame, Ameeleza Dendego. 

Ameeleza kuwa maeneo yote ya miradi ambayo yana migogoro lazima Viongozi wakae wahusika ili kuondoa changamoto hizo kwa wakati nia ikiwa ni kuona wananchi wanaanza kupata huduma bora na za msingi karibu na maeneo yao.

Dendego pia amepongeza hatua zinachukuliwa na Watendaji katika kusimamia na kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo ili iweze kutekelezwa kwa viwango na ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga amemhakikishia Mkuu wa mkoa wa Singida kuwa atahakikisha miradi yote inayotekelezwa mkoani humo inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa.

Dkt. Mganga amewasisitiza Watendaji wote washiriki kikamilifu katika kusimamia miradi iliyopo kwenye maeneo yao ili wananchi waweze kufurahia huduma bora zinazotolewa na Serikali yao.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe, ameeleza kuwa atafanya kazi kwa usiku na mchana kwa ushirikiano na Watendaji wengine ili kuhakikisha miradi yote ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye Wilaya yake inakamilika hadi mwisho wa mwezi huu kama maelekezo ya Serikali yanayotaka.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.