Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewahimiza Watanzania kununua na kutumia bidhaa zinazotengenezwa na Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) nchini ili kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.
Mkuu wa mkoa wa SINGIDA ametoa wito huo katika Mahafali ya wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi RC Mission VTC wilayani Manyoni mkoani Singida alipokuwa akizungumza na wahitimu, wanafunzi, wazazi na viongozi mbalimbali wa Serikali ya halmashauri ya wilaya ya Manyoni waliohudhulia Mahafali hayo.
Mahafali ya wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi RC Mission VTC, Wilayani Manyoni mkoani Singida, yaliambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanafunzi hao ikiwemo fanicha, nguo mbalimbali (batiki), pamoja na huduma za magari na umeme.
Kwa upande wao wahitimu wa chuo cha ufundi stadi RC Mission VTC wameiomba Serikali ya halmashauri ya Manyoni kuwatambua wanafunzi hao kwa kazi nzuri wanazofanya.
Jumla ya wanafunzi 49 wamehitimu mafunzo ya Ufundi Stadi kati ya hao wasichana waliohitimu ni 4, suala ambalo Dktr. Rehema Nchimbi amesema wasichana wanapaswa kutambua nao wanahaki sawa kama ilivyo kwa wanaume, na kuahidi kuwalipia ada wanafunzi wa kike 3 kwa fani ya umeme 1 na ufundi magari 2, ikiwa kama motisha kwa wengine.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.