Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge hivi karibuni amekutana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia maandalizi ya Ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) ambacho ni Kampasi ya Singida.
Wakiwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Naibu waziri huyo amasema lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli za Ujenzi wa chuo hicho na kutembelea shughuli za TASAF zinazoendelea Wilayani Manyoni.
Amesema Chuo hicho kitakuwa ni msaada mkubwa kwa watu wa Singida na maeneo mengine huku alibainisha kwamba uchumi utapanuka na ajira zitaongezeka.
Kwa upande wake RC. Mahenge ameshukuru Ujenzi wa chuo hicho na kusema ni hatua kubwa ya maendeleo kwa Mkoa huo.
Aidha amemuomba Naibu waziri huyo kushughulikia changamoto ya watumishi wa Mkoa huo ambao wamekuwa wakikaimu kwa muda mrefu pasipo kuthibitishwa.
Hata hivyo RC akamueleza Naibu Waziri huyo changamoto ya uhaba wa walimu na madaktari Katika Mkoa huo huku akibainisha kwamba ongezeko la madarasa na vituo vya Afya vilivyomalizika hivi karibuni kumeleta uhitaji mkubwa wa walimu na manesi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali wakiwa katika ofisi ya ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa ziara
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.