Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 139 katika Magereza ya mkoa huo wakati alipokuwa akiwatoa wafungwa hao walioachiwa kwa msamaha wa Rais katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Muungano.
Dkt. Nchimbi ameyasema hayo Desemba 10, 2019 alipokuwa katika Gereza la mkoa alipofika kutekeleza agizo la Mhe. Rais kuwaachia wafungwa hao waliopata msamaha huo.
“Tunashukuru kwa Sababu sisi wana wa Singida tumenufaika kwa msamaha wa wafungwa 139 ni wengi sana, Mheshimiwa Rais alipokuwa akitangaza msamaha huo kati ya maneno aliyoyasema hataraji kwamba ‘mnapotoka hapa leo muende mkarudie makosa’ mkirudia makosa adhabu mtakayoipa ni kubwa sana, hatarajii mfanye makosa” Dkt. Nchimbi
Aidha mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Magereza Msepwa Omary, ameyataja Magereza yaliyotoa wafungwa hao kuwa ni; Gereza la Singida wafungwa 60, Manyoni 37, Kiomboi Iramba 27, Ushora 15, kati ya hao, 136 ni wakiume na 3 wafungwa wakike.
Nao baadhi ya wafungwa walioachiwa huru wamemshukuru sana Mheshimiwa Rais Magufuli kwa msamaha aliotoa na kuahidi uhuru walioupata kufanya kazi kwa bidii katika kujenga uchumi wa familia na Taifa kwa ujumla.
Aidha wameushukuru uongozi wote wa Serikali ya mkoa wa Singida sambamba na askari wote walioshirikiana nao wakati wote walipokuwa kifungoni.
Zoezi hilo limeenda sanjari na utoaji wa vyeti uliofanywa na Mkuu wa mkoa Dkt. Rehema Nchimbi kwa wafungwa wote 139 walioachiwa huru.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.