Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameongoza mkutano maalum wa Baraza la waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, kujadili majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2018.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt. Nchimbi ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kuwa na Hati Safi na kuwataka watumishi, watendaji pamoja na wataalamu kuendelea kuwatumikia kikamilifu wananchi wao vijijini.
"Hati safi inamaana kwamba, sio tuu taarifa za kwenye makaratasi bali tafsiri yake kubwa ni udhihirisho wa hali halisi kwa yale yanayotekelezwa na halmashauri na ambayo yatadhihirika katika mabadiriko chanya ya maisha ya wananchi" Alisema Dkt Nchimbi
Aidha, Dkt. Nchimbi amewataka watumishi, watendaji, pamoja na wataalamu kusimamia kila jambo linalohusu maendeleo ya wananchi wa halmashauri ya Ikungi bila kuangalia itikadi za vyama pamoja na kulinda misitu na kuwasihi waheshimiwa Madiwani kusimamia kwa nguvu zote uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti ovyo unaofanywa kwa ajili ya matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.
"Niwaombe, mlinde misitu, msifanye mdhaa wowote na ulinzi wa misitu yetu. Niwaombe waheshimiwa Madiwani tudhibiti sana uchomaji wa mkaa" - Dkt. Nchimbi
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.