Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida umeokoa Sh.Milioni 100 katika ujenzi wa mradi wa maji kwenye kijiji cha Senene Wilayani Mkalama kutokana na kutumia Mkandarasi wa ndani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, alisema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo kwenye kijiji hicho ambao makadirio ilikuwa ugharimu zaidi ya Sh.milioni 570 lakini zimetumika chini ya hizo na hivyo kuokoa Sh.milioni 100.
Alisema namna bora ya kuishukru Serikali ni kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa zaidi ya miaka 25 na jukumu la kuulinda ili usiweze kuharibika ni la kila mwananchi.
“Rais wetu wa Awamu ya Sita anawajali sana wananchi wake na anawekeza kwenye maisha ya watu, leo tunaenda kuzinduza miradi ya maji minne ambayo zaidi ya karibia Shilingi Bilioni 1.5 zilitumika kutatua tatizo la maji Wilaya moja tu ya Mkalama. Alisema RC Serukamba”
Serukamba alisema RUWASA wahakikishe maeneo yote yanayotoa huduma kwa wananchi katika Wilaya ya Mkalama kama vile shule, vituo vya afya, Polisi maji yapelekwe ili kuondoa changamoto ya maji kwenye maeneo hayo.
Aidha, aliwataka wazazi na walezi wenye watoto waliofikisha umri wa kwenda shule wawaandikishe kabla ya Disemba 30 mwaka huu ili waweze kuanza darasa la kwanza 2023.
"Nawaomba wazazi pelekeni watoto wenu wakaandikishwe shule, hadi sasa ni asilimia 49 tu ya watoto waliofikia umri wa kuanza shule Mkoa wa Singida ndio wameandikishwa," alisema.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo, alisema kati ya vijiji 70 vilivyopo katika Wilaya hiyo 63 vinapata huduma ya maji safi na salama na hivyo kufanya upatikanaji wa maji katika Wilaya kufikia asilimia 80.
Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mkalama, Antidius Mchunguzi, alisema mradi huo ulikuwa ugharimu zaidi ua Sh.milioni 569 lakini kutokana na kutumia mkandarasi wa ndani hadi kukamilika umegharimu Sh.milioni 475.
Mchunguzi alisema kukamilika kwa mradi huo kumeongeza kiwango cha asilimia 1.5 cha upatikanaji wa maji katika wilaya ya Mkalama na hivyo utapunguza muda wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Senene.
Alisema faida nyingine za mradi huo ni kwamba utapunguza migogoro kwenye familia na kuongeza uchumi kwa wananchi.
Mheshimiwa Mbunge Francis Isack akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa miradi ya maji wilayani Mkalama
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.