Wilaya ya Ikungi imefanya semina ya kuwajengea uwezo wataalamu viongozi na jamii kutoka katika kata za mradi wa JPRWEE unaohusu uhifadhi wa jamii na bajeti zenye mrengo wa kijinsia.
Hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Novemba 6,2024.
Akifungua mafunzo hayo,Mkurugenzi Mtendaji Ndg Justice Kijazi amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanawake kiuchumi, Usawa wa kijinsia katika maendeleo na umiliki wa ardhi.
"Mambo kama vile mgawanyo wa kazi, mgawanyo sawa wa rasilimali, kuepukana na mila potofu, ubaguzi wa kijinsia ni vitu vinavyopaswa kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuepukana na migogoro ya kijamii" amezungumza Kijazi
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Bi Haika Massawe ameongeza na kusema kuwa kuna haja ya wanawake kuwezeshwa kiuchumi ili kuongeza fursa za kazi zenye malipo, kuwajengea uelewa wa haki zao pamoja na kuwapa elimu mtu mmoja mmoja na kaya kwa ujumla.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.