Serikali imeahidi kutoa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima mbali mbali wa zao la pambamkoani Singida kuanzia msimu huu wa kilimo ikiwa ni moja ya juhudi za kuhamasishana kufufua kilimo hicho mkoani hapa.
MkurugenziMkuu wa Mamlaka ya Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga ameeleza hayo juzi katikavijiji vya Kinyangiri na Lyelembo wilayani Mkalama katika siku ya kwanza yaziara yake ya siku mbili kuhimiza Kilimo cha pamba mkoani Singida.
Kwamujibu wa Mkurugenzi huyo, Kampuni ya Biosustain iliyopo mjini hapa imepewajukumu la kuleta na kusambaza mbegu na madawa yote yahusuyo kilimo cha pambabure na kwamba gharama ya pembejeo hizo italipwa na Serikali.
Kutokanana hilo, Mkurugenzi huyo amewataka Wakulima kutumia vyema fursa hiyo kwa kulimamashamba makubwa zaidi lakini pia kwa kuzingatia tija na ubora wa pamba.
Amesemakuwa Wakulima wataweza kufanya hivyo tu iwapo pia watawatumia kikamilifuwataalamu wao wa kilimo na kufuata Kanuni na Taratibu za kilimo bora.
“Mmepewaupendeleo maalum, kazi yenu sasa ni kulima tu, malipo ya mbegu na viuatilifuvyote italipwa na Serikali. Hapa hakuna kisingizio cha kushindwa kulima”, amesemaMtunga na kuongeza;
“Pandenivizuri ili wakati mnatumia dawa, kiwango kikubwa cha dawa kisipotee bure maanakama hukupanda kwa mstari lazima kutakuwa na ugumu wa kupulizia mimea yako.Jengeni utamaduni wa kuwatumia wataalamu wa kilimo kama ilivyo kwa wafugajimifugo yao inapopatwa na maradhi”.
Aidha,amewataka wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanang'oa masalia yote ya misitu yapamba na kuichoma moto kwa kuwa, kwa kuacha kufanya hivyo wanaruhusu waduduwaliomo kwenye masalia kuendelea kunenepeana na hivyo kuhatarisha mazao mapyayanayopandwa.
Mkurugenzihuyo amewasihi wakulima kuacha kuchanganya kilimo cha pamba na mazao mengineakisema kuwa tafiti zinaonesha pamba iliyochanganywa na mazao mengine hutoavitumba vitatu tu ikilinganishwa na vitumba 10 kwa kilimo cha pamba iliyolimwapeke yake.
Wakulimawa zao hilo wamemueleza Mkurugenzi huyo kuwa, moja ya sababu za kushuka kwauzalishaji pamba kwenye maeneo yao ni pamoja na bei kuwa ndogo kwa kisingiziocha Soko la Kimatafa kushuka na kuchezewa mizani wanazotumia kupima mazao yao,hali inayowapunja kimapato.
Hatahivyo, wamejibiwa kuwa suluhisho la kuchezewa mizani lipo mikononi mwao ilimradi tu wajenge tabia ya kuhoji mara moja wanapoona mambo yanaenda isivyobadala ya kusubiri hadi siku ya vikao.
Wakatihuohuo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewataka watendaji wote waserikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Singida kulima ekari moja ya pambakila mmoja ili kuamsha hamasa kwa wananchi wengine.
DktNchimbi ameongeza kwa kuwataka watendaji hao kuliweka zao la pamba kama ajengakatika vikao vyao, huku akiwataka viongozi wa dini na vikundi vya kwayakuonyesha mfano kwa kulima vizuri pamba.
Ameongezakuwa vijana wanaocheza vijiweni ‘pooltable’ waache mara moja na kujikita katikakilimo cha pamba kwa kuwa ni chanzo kikubwa na cha uhakika cha kujipatia fedhana hivyo kuchangia kukuza uchumi.
Aidhaamewataka wakulima wa pamba kuwasikiliza wataalamu na sio kupanda kwa mazoeahuku akishauri kuwa mikutano yote inayohusu kilimo cha pamba ifanyike katikamashamba ya wakulima.
DktNchimbi ameeleza kuwa kauli mbiu mpya ya kilimo cha pamba kwa Mkoa wa Singidani, ‘Singida Mpya, kwa Pamba yenye Tija’.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.