Serikali imejipanga kuinua uzalishaji wa zao la alizeti katika Mkoa wa Singida kwa kuwakopesha wakulima mbegu aina ya Record ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuondoa uhaba wa mafuta ya kula ambao umekuwa ukijitokeza kila mwaka.
Akiongea wakati wa ziara yake leo Wilayani Singida Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema wataikabidhi Halmashauri hiyo tani 100 za mbegu za alizeti standerd seed ambapo wakulima watakopeshwa.
Mkopo huo wa mbegu za ruzuku zinazogharimu kiasi cha shilingi 3500 kwa kilo MOJA watazirejesha kwa Halmashauri husika baada ya kuvuna mazao yao na kuyauza. Alibainisha Bashe.
Naibu Waziri huyo amefafanua kwamba wakati wa ugawaji wa mbegu hizo maafisa kilimo wahakikishe kila mkulima anaandika jina, Kijiji alichotoka, namba ya simu ukubwa wa shamba alilolima na kiasi cha mbegu alichopewa na kusaini.
Aidha Mhe. Bashe ameagiza Halmashauri kuhakikisha makampuni yote yatakayonunua mbegu za alizeti kuhakikisha wanatoa huduma za ugani kwa wakulima watakao wazalishia na kuhakikisha eneo lililopata huduma hizo linauza kwa makampuni husika.
Amewaomba viongozi wa siasa kuhakikisha wanasimamia ugawaji wa mbegu kwa wakulima, usimamizi wa mashamba pamoja na makampuni yatakayoonesha nia ya kushirikiana kwa namna yeyote na wakulima ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa alizeti.
Hata hivyo akawataka Maafisa ugani kuhakikisha msimu ujao wa kilimo wa mwaka 2022/23 wanakuwa na taarifa za kila Kata kuhusu aina ya mazao yanayostawi eneo hilo na aina ya mbolea itakayohitajika ili wakulima waweze kulima zao zaidi ya moja.
Wizara ya kilimo itatoa vitendela kazi vikiwemo mashine za kupimia udongo kwa kila Hamashauri ili kurahisisha zoezi hilo, alieleza Naibu Waziri.
Amesema wakulima wanapaswa kulima mazao mbalimbali yenye thamini kubwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi kwa lengo la uimarishaji wa usalama wa chakula kwa kila mkulima na kuongeza kipato alisistiza Mhe. Bashe
Hata hivyo Naibu Waziri alieleza kwamba Wizara ya kilimo kupitia Wakala wa mbegu za kilimo (ASA) imeweka mikakati ya kuzalisha mbegu nyingi za kisasa katika msimu wa 2022/23 ili kurahisisha upatiakanaji wa mbegu.
Awali Naibu Waziri huyo ameahidi kuwatuma wataalamu wa umwagiliaji kutoka wizarani waungane na wenzao wa mkoani wakafanye tathmini katika skimu zote za Mkoa wa Singida na kuchagua baadhi ambazo zitakarabatiwa kwa asilimia miamoja ili kuleta matokeo makubwa katika kilimo.
Amesema mkoa mzima wa Singida una skimu za uwagiliji zenye jumla ya ukubwa wa hekta 3,450 lakini hekta zinazo tumika ni 100 tu ambazo ni chini ya asilimia kumi jambo ambalo haliewezi kuleta mabadiliko makubwa ya katika kilimo.
“Lazima tuondokane na kilimo cha kubahatisha, ili tuweze kukifanya kilimo kiwe cha ki biashara ni lazima tuingie kwenye kilimo cha umwagiliaji na tutafute namna ya kutunza miuondombinu kwa kulipa tozo kidogo itakayosaidia kurekebisha miundombinu hiyo”. Alisema Bashe.
Katika ziara hiyo Naibu waziri aliweza kutembelea skimu ya uwamgiliaji iliyoko Kijiji cha Msikii Kata ya Mughamo yenye hekta 150 zinazofaa kwa umwagiliji na Kijiji cha Msange chenye hekta 1,400 ambapo chanzo cha maji ni bwawa lianalohitaji ukarabati na uchimbaji wa visima .
Akiwa maeneo hayo Naibu waziri huyo ameongea na wakulima wa vitunguu na mahindi ambapo kupitia wakala wa mbegu ASA ameahidi kuwaletea mbegu ya mahindi aina ya stuka waifanye kama majaribio lengo likiwa ni kuwafanya wakulima hao kulima kilimo cha mazao mbalimbali.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Mhandisi Paskasi Muragili amesema Hamashauri hiyo imejipanga kikamilifu kutekeleza maagizo ya Serikali kuanzia yote yaliyotolewa na Waizri Mkuu yanayohusu uendelezaji wa zao la alizeti na mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mafuta nchini.
Amesema wilaya ya Singida mwanzoni walikuwa na wakulima 8,546 wa alizeti ambao walilima hekta 21,000 na kuvuna tani 36,222 lakini baada ya maagizo ya Serikali wametoa elimu na hamasa wakulima 21,000 wamejiorodhesha kulima hekta 38,000 kwa wakulima wadogo na Taasisi 438.
Amesema wilaya hiyo inategemea kuzalisha tani Zaidi ya 94,000 kwa msimu ujao ambapo ni mara mbili zaidi ya msimu uliopita.
Mtendaji wa Kata ya Mughamo Katika Halmashuri ya Wilaya ya Singida Bw. Clement Njou akisoma taarifa fupi ya shughuli za kilimo katika Kata hiyo.
Mkuu Wilaya ya Singida Paskasi Muragili (kulia) akiwa ameshikili zawadi ya miwa walipewa na wanakijiji cha Msikii, wapili kutoka kulia ni Naibu Waziri Bashe
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Hussein Bashe (kulia) akiwa katika shamba la mbegu za vitunguu
Muonekano wa eneo la bonde lililopo Kata ya Mughamo katika Halmashuri ya Wilaya ya Singida
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.