Serikali itaendelea kusimamia utoaji wa matibabu kwa Wazee bila malipo, upatikanaji wa dawa Hospitalini na uwepo wa dirisha maalum kwa ajili ya Wazee ili kuwaenzi na kuwaondolea usumbufu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Singida Mjini Mhandisi Paskasi Muragili kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Singida wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wazee Duniani yaliyofanyika mjini Singida.
Amesema Serikali itaendelea kutoa huduma kwa wazee pasipo kuchangia gharama za matibabu na kuboresha changamoto ambazo zimejitokeza katika utoaji wa huduma hiyo kwa kundi hilo.
"Sisi sote ni mashahidi wa utolewaji wa huduma za Afya bila malipo kwa Wazee wote. Nitoe wito kwenu kufika kwenye vituo vya huduma za Afya vya Serikali ili kupatiwa huduma bila kuchangia gharama za matibabu".
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo kuendelea kuwachangia wazee wasio na uwezo na kuwaunganisha kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) na wale wenye uwezo wa kujiunga wenyewe amewahamasisha wajiunge ili kuendelea kuboresha huduma za Afya.
Awali Mwenyekiti wa umoja wa Wazee hao SAWATA Bw. Ramadhani Juma Moghu ameishukuru Serikali kwa hatua walizoendelea kuzichukua katika kuimarisha Sekta hasa kwa wazee.
Akijibu hotuba ya wazee hao Mkuu huyo wa wilaya amewataka Maafisa maendeleo ya jamii wa kila Halmashauri kuwashauri wazazi ambao watoto wao wanaolelewa na wazee kuona umuhimu wa mtoto kuishi na mzazi ili kuwapunguzia majukumu.
Amesema Wazee wengi wameachiwa watoto na watoto wao au wajukuu. Malezi ya watoto hao ni jukumu la wazazi wao hivyo ni vema tukawaelimisha watoto na wajukuu zetu juu ya umuhimu wa malezi ya Wazazi kwa watoto. Alisistiza Muragili
"Kwa kuwa kila Halmashauri kuna Ofisi za Ustawi wa Jamii niwaombe mfike ili wazazi hawa waweze kuwajibika kama Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 inavyoelekeza".
“Nitoe shukrani kwa viongozi wa Baraza la Wazee mkoa na Viongozi wa SAWATA katika kufanya maandalizi na kufanikisha maadhimisho haya. Aidha, nazishukuru Taasisi zote zilizoweza kutoa michango yao ya hali na mali katika kuwezesha maadhimisho haya”. Alimalizia Muragili.
Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Mhandisi Paskasi Muragili (kulia) akitembalea banda la Wazee wajasiriamali katika
maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika leo mkoani Singida
Mwenyekiti wa umoja wa Wazee hao SAWATA Bw. Ramadhani Juma Moghu akisistiza jambo wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Mhandisi Paskasi Muragili (kulia) akikabidhi Mwongozo wa majukumu ya Mabaraza ya Wazee ngazi ya vijiji, mtaa, kata, wilaya na mkoa na Taifa kwa viongozi wa Mabaraza wakati wa madhimisho hayo
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwalimu Dorothy Mwaluko (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa umoja wa Wazee hao (SAWATA) muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika leo mkoani Singida
Burudani zikiendelea
Picha ya pamoja
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.