• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SERUKAMBA AWAPA MAAGIZO WAHANDISI

Posted on: September 19th, 2023

WAHANDISI katika Mkoa wa Singida wanao simamia madarasa ya mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) wametakiwa kuhakikisha wanawasimamia Wakandarasi wanaojenga miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Maagizo hayo yametolewa leo tarehe 19 Septemba, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa hatua za kukamilika miradi hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Manyoni na Itigi mkoani humo.

Serukamba amesema kuwa inawezekana Wahandisi wa baadhi ya halmashauri husika wanaweza kuwa ni chanzo cha kuchelewesha kukamilika kwa miradi hiyo kutokana na kutokuwa na desturi ya kwenda kwenye maeneo ya kazi kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya kazi zinazofanywa na Wakandarasi waliopewa kazi hizo.

Amesema kuwa kazi za Wahandisi wa halmashauri ni kuhakikisha wanatembelea maeneo ya kazi kwa nia ya kuwakagua Wakandarasi, kuwasimami, kuwashauri, kuwapangia majukumu na kuona hatua za utendaji kazi zinavyoendelea pamoja na kiwango cha utendaji ili kuharakisha ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule kutekelezeka kwa ufanisi.

Serukamba akiwa kwenye ziara hiyo ya kikazi kwenye halmashauri mbalimbali ndani ya Mkoa huo amewataka Waandisi wa halmashauri ambako miradi hiyo inatekelezwa kuhakikisha ifikapo tarehe 30 Septemba mwaka huu miradi yote iwe imekamilika.

Sambamba na hilo amewataka Watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanatembelea miradi hiyo kila siku na kukusanya taarifa kila jioni ili kuona ni Mkandarasi gani ambaye anakwamisha miradi hiyo na ikibidi anyang'anywe mradi na kupewa mtu mwingine ambaye anaonesha nia ya kumaliza kazi mapema.

Serukamba amesema Mkandarasi ambaye anafanya kazi kwa kusuasua na kufanya kazi chini ya kiwango hatavumiliwa kwani ni lazima thamani ya fedha ionekane na miradi iishe kwa wakati ili walengwa waweze kutumia madarasa hayo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.