• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SINGIDA TUMEFIKISHA MADAKTARI BINGWA KWA WANANCHI NA ZOEZI HILO NI ENDELEVU; DOKTA NCHIMBI.

Posted on: March 22nd, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi ameagiza Kliniki tembezi ya huduma za kibingwa kwa mkoa wa Singida kuwa endelevu huku akizielekeza halmashauri kuandaa mpango wa utekelezaji wa zoezi hilo kwakuwa linagusa maisha ya wananchi wa hali ya chini.Dokta Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Iambi Wilayani Mkalama ambako zoezi la kliniki tembezi ya madaktari bingwa wa fani nane kwa Mkoa wa Singida lilikuwa linahitimishwa.

Amesema mara baada ya kukamilika kwa halmshauri zote saba mpango wa kuanza kutoa huduma za kibingwa kwa awamu ya pili uanze mara moja kwakuwa wagonjwa wengi walionufaika ni wale webnye kipato duni na walikuwa wameshakata tama ya kupata matibabu.Dokta Nchimbi ametembelea wodi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji na daktari bingwa wa wanawake, wodi ya akina baba waliofanyiwa upasuaji wa magonjwa ya tezi dume na matatizo ya njia ya mkopo pamoja, ametembelea chumba cha upasuaji wagonjwa wa macho na kumalizia wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mfumo wa upumuaji na midomo sungura.

Amesema, “Ukisikiliza ushuhuda wa wagonjwa waliopatiwa matibabu ya kibingwa utaona umuhimu wa kliniki tembezi, wengine walikwisha kata tamaa ya kuishi na kusubiria kifo, wengine walitengwa na kusimangwa, kuna mmoja wakati analetwa hospitali kuonana na madaktari hawa majirani waliwaambia ndugu zake watarudisha maiti lakini amepona kabisa”.

Akitoa taarifa ya  kliniki tembezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta John Mwombeki amesema wagonjwa walioonwa na madaktari bingwa kwa muda wa siku nne ni 675 na waliofanyiwa upasuaji ni 71.

Dokta Mwombeki ameeleza kuwa kliniki tembezi imekuwa na manufaa kutokana na kuwa na gharama nafuu kuliko hospitali kubwa za rufaa ambapo wagonjwa wengi wameshindwa kufika huko.Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Injinia Geofrey Sanga ameeleza kuwa halmashauri yake imetoa milioni 18 kufanikisha zoezi hilo na kuahidi kuendelea kushikiana na Mkoa katika awamu ya pili ili wananchi wote wenye uhitaji wa huduma za madaktai bingwa wazipate.

Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani, madaktari bingwa wanawake, wototo, macho, upasuaji, mifupa na njia ya mkojo wametoa huduma za kibingwa wilayani Mkalama kuanzia Februari 27 hadi Machi 3.Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Singida amezindua rasmi kilimo cha korosho kwa kushiriki zoezi la upandaji wa mikorosho na mihogo na kuhamasisha wananchi kupanda mikorosho hasa katika mashamba yao waliyolima mihogo.Dokta Nchimbi amesema korosho ni zao linaloweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka hamsini na pia ni rafiki wa mazingira, huku akiendelea kusisitiza kilimo cha viazi lishe kwakuwa ni mkombozi wa uchumi wa wananchi wa Singida.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.