• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Singida waadhimisha sikukuu ya Muungano kwa kufanya usafi

Posted on: April 26th, 2022

Wafanyabiashara wa vitunguu mkoani Singida leo wamepigwa marufuku kutumia  matumizi ya vifungashio ambavyo havijathibitishwa na Serikali na ambavyo vinazidi kilo mia kwa kuwa vinawapunja wakulima.

Akiongea na wafanyabiashara katika soko la vitunguu lililopo Kata ya Misuna mkoani hapo wakati wa zoezi la kufanya usafi Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Pasksi Muragili amewataka wafanyabiashara katika soko hilo kuachana  na matumizi ya vifungashio ambavyo havijathibitishwa na Serikali badala yake watumie vifungashio aina ya neti.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Pasksi Muragili akizungumza na Wananchi walioshiriki katika zoezi la usafi kusheherekea Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 26, 2022

Amewataka viongozi wa Soko hilo kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaotumia vifungashio vyenye ujazo wa magunia unaozidi kilo Mia moja maarufu kama rumbesa kwa kuwa unawapunja wakulima.

"Serikali ilishatoka muongozo kuhusu matumizi sahihi ya vifungashio lakini nimepata taarifa kwamba bado wafanyabiashara wanaendelea kutumia viroba na magunia ambayo ni zaidi ya kilo Mia naomba kuanzia leo asiwepo mfanyabiashara anayetumia kifungashio zaidi ya neti ambayo imekubalika. Tunafanya hivi ili kuwasaidia wakulima wetu" Mhandisi Muragili.

Awali akihutubia wananchi walioshiriki shughuli za usafi katika soko hilo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Muungano amesema zoezi hilo liwe endelevu na kila mtu awe na kawaida ya kufanya usafi katika maeneo yanayo wazunguka.

Mhandisi Muragili amebainisha kwamba Mkoa umejipanga kuhakikisha inaongoza kwa usafi hapa nchini na ndilo dhumuni la kuhakikishia usafi unafanyika kila siku.

Katika kuhakikisha zoezi linafikia lengo Mhandisi Muragili amemtaka Mkandarasi anayehusika na uzoaji la taka kuhakikisha wanaondoa vizimba vya taka kabla ya kufikia saa nae mchana wa leo.

Amesema anafahamu kwamba Mkandarasi anayesafisha eneo hilo la soko ana vitendea kazi vingi ikiwemo magari lakini hana vijiko kwa ajili ya kuzolea taka hivyo kumtaka akatafute ufumbuzi juu ya hilo ili aweze kusaidia kufikia lengo la kuweka Safi Mkoa.

Alimalizia hotuba yake DC Muragili akawataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano tarehe 28 Aprili 2022.

Amewataka wananchi kushiriki zoezi hilo na kuwataka kuupuzia uvumi unaosemwa katika mitandao ya kijamii kwamba chanjo hiyo ina madhara, amesema wataalamu wa afia wamejiridhisha kwamba chanjo hizo ni salama kwa watumiao na inayoletwa kwa matone kwa watoto wote waliyopata au ambao hawajapata chanjo hiyo.

Amesema zoezi la chanjo hiyo limetokana na uwepo wa waathirika wa Polio katika nchiza jirani hivyo Serikali imeamua kuchukua tahadhari kwa kuwachanja watu wake ili kuepusha tatizo hilo. Alibainisha DC Muragili.

Alimalizia hotuba yake DC huyo amewataka wananchi wote kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23 Agost 2022.

Naye Mwenyekiti wa Soko la vitunguu Misuna Iddy Swalehe Mwanja akatumia nafasi hiyo kuiomba Wizara ya Kilimo pamoja na viwanda na Wizara ya viwanda na Biashara kusimamia zoezi la upatikanaji wa vifungashio vya kutosha uwezo wa kubeba kilo Mia moja kwa kuwa imeoneka kutopatika katika baadhi ya mikoa.

Amesema Singida wapo tayari kutumia vifungashio vya neti ambavyo havimpunji mkulima lakini ipo mikoa bado inaendelea kutumia rumbesa hivyo kusababisha wengine kukosa soko la vitunguu.

Mwenyekiti wa Soko la vitunguu Misuna Iddy Swalehe Mwanja akizungumza mara baada ya zoezi la usafi lililofanyika katika soko hilo.

Swalehe ameendelea kuiomba Serikali kuyasimamia vizuizi vilivyopo barabarani kusimamia kikamilifu ukaguzi wa rumbesa ili kusaidia kuondoa changamoto za ujazaji wa bidhaa  wa kupitiliza.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali ya Serikalini pamoja na viongozi wa Soko na Wananchi mbalimba walikuja kufanya usafi wa maeneo hayo.

Muonekano wa vitunguu vilivyofungashwa kwa usahihi kwaajili ya uuzwaji.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.