Ajira Zaidi ya 190 za moja kwa moja na ajira 400 zisizo za moja kwa moja zinatarajiwa kunufaisha wakazi wa Mkoa wa Singida huku wakulima zaidi ya 26000 kunufaika na mradi wa kiwanda cha mafuta cha Wild Flower Grains&Oil Mill Company Limited kupitia uwekezaji mkubwa wa kimkakati uliokamilika kwa asilimia 95 mpaka sasa.
Mhe.Jerry Silaa Waziri wa habari na mawasiliano na teknolojia ya habari,alipotembelea kiwanda hicho leo hii amesema ni wakati sasa wa Tanzania kupunguza kuagiza bidhaa nje ya nchi kwani maendeleo ya viwanda yatarahisiaha uchakataji,na upatikanaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo mafuta ya kupikia ambayo yatainua maisha ya wengi katika mchakato wa kupata malighafi kutoka kwa wakulima wa mazao,wasafirishaji mazao,na wauzaji wa bidhaa za kiwandani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego akizungumza katika ziara hiyo amewakaribisha wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Singida kwani ni mahali salama na upatikanaji wa umeme na mazao ya biashara kama alizeti na vitunguu.
Amesisitiza wawekezaji wa ndani kujitokeza kayika kuwekeza katika fursa hizo za biashara kwa kuiga mfano wa wawekezaji wazawa wa kiwanda hocho cha mafuta kwani wamethubutu na wameweza kuifanya Singida kupiga hatua katika maendeleo ya viwanda.
"Wawekezaji wa ndani waje kujifunza hapa kwetu Singida kwani wataalam wetu wote katika kiwanda hiki kuanzia ujenzi wa msingi wa kiwanda hiki ni vijana wetu wazawa wa hapa hapa Tanzania wakitengeneza bidhaa na kuendesha mashine"
Akiwasilisha taarifa ya mradi wa kiwanda hicho cha mafuta Jamal Shaban,amesema kuwa mipango ya baadae ya kiwanda hicho ni kufanya utanuzi wa kiwanda na kuongeza mashine za kusaga mahindi ili kupata unga na kuongeza mashine za kukoboa mpunga ili kupata mchele kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa hapa nchini ili kuweza kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani.
"Kwa kuongeza mashine za kusaga na kukoboa mahindi na mpunga tutaongeza thamani ya mazao yetu yanayozalishwa hapa nchini na kuuza bidhaa bora zilizoongezwa thamani".alisema Jamal
Wamiliki wa kampuni inayotekeleza nradi huo ni wazawa wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 18 katika uwekezaji wa miradi ya kilimo na viwanda huku mradi huo ukiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 63 wakiwa na uwezo wa kusaga tani 225 za mbegu za alizeti kwa siku ikiwa matarajio ya uzalishaji wa mafuta kwa siku ni tani 75 na tani 2,250 kwa mwezi ambayo yatauzwa ndani na nje ya Mkoa wa Singida.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.