• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Singida yapokea mbegu 20,000 za Mkonge

Posted on: December 2nd, 2021

Mkoa wa Singida umepokea  mbegu za mkonge miche 20,000 itakayogawiwa kwa wakulima wa wilaya ya Singida Vijijini ikiwa ni mpango wa kuongeza chanzo cha mapato kwa mkoa huo na wananchi kwa ujumla.

Akipokea mbegu hizo leo Desemba 3.2021 kutoka Bodi ya Mkonge Tanzania Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge amesema zao la mkonge ni utajiri mwingine ambao umeingia mkoani Singida na wataalamu wamekiri ardhi ya mkoa huo kustawisha mkonge ambao ni mrefu na haushambuliwi na magonjwa.

Amewataka wakulima mkoani hapo kulima mazao yanayovumilia ukame kama alizeti, mtama, mkonge na dengu kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa mvua kunyesha chini ya kiwango kwa mwaka huu.

Awali akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) Dkt. Mahenge akatumia muda huo  kuwaasa wananchi wote wa Singida kulima mazao yanayovumilia ukame na ya muda mfupi ili kukabiliana na hali ya hewa ya sasa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mhanddisi Pasikas Muragili akabaniisha kwamba uzalishaji wa mkonge unafanyika  katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na unafanyika katika mapalio (mipaka ya mashamba) iliyopandwa mkonge na kuuchakata.

Amesema wakulima wilayani humo wameanzisha AMCOS inayofahamika kwa jina la Mpipiti katika kijiji cha Mpipiti ambao wana mashine 16 za kuchakata mkonge na kati ya hizo mashine 10 ni za wanachama  na sita ni za watu binafsi.

Aidha wilaya imeandaa mashamba yenye ukubwa wa ekari 100 ambapo ekari 50 ni kwa ajili ya waanzilishi wa zao hilo na 50 kwa ajili ya wakulima wengine wa wilaya hiyo alibainisha DC Muragili.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Bodi ya Mkonge  Saady Kambona wakati akikabizi  mbegu hizo amesema kuanzia sasa Singida inaingia kwenye mikoa mitatu ya uzalishaji wa mkonge ambayo ni Tanga, Morogoro na Singida.

Amesema zao la mkonge halina msimu  maalum muda wote linastawi hivyo  kuwaomba wakulima wa mkoa huo kutumia fursa hiyo hasa wakati huu ambapo mbegu zinagawiwa bure na serikali.

Kambona  amesema matumizi ya zao hilo yamekuwa yakiongezeka kila mwaka  ambapo kwa sasa unatumika kutengeneza mbao kwa ajili ya kutengeneza thamani, sukari, nyuzi, kamba na kwenye magari.

Hata hivyo ameahidi  kuleta mbegu 165,000 za mkonge ambazo zitatosheleza katika mashamba yenye ukubwa wa ekari 100 zilizitengwa wilayani Singida Vijijini.

MATUKIO KATIKA PICHAKatibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akiwapitisha wajumbe kwenye muhtasari wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) -Singida

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) -Singida

Sekretarieti ya Mkoa wa Singida wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) -Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) -Singida (Kulia kwake ) Katibu Tawala Mkoa Dorothy Mwaluko.

Habari zaidi tembelea: http://singidars.blogspot.com/2021/12/singida-yapokea-mbegu-20000-za-mkonge.html

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.