Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba, leo amelitahadharisha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Singida kwamba yupo tayari kuingia kwenye mgogoro na yeyote ambaye atasababisha hoja za CAG kutofungwa, kulegalega kwenye makusanyo na kutofuatilia miradi ya maendeleo.
RC Serukamba ametoa tahadhari hiyo wakati wa Mkutano wa Baraza la maalum la Madiwani la Manispaa ya Singida lililoketi ili kupitia hoja za CAG Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ambapo zimefungwa hoja 20 kati ya hoja zilizoibuliwa.
RC Serukamba amesema Manispaa hiyo ina uwezo mkubwa wa mapato ambapo ameeleza kuwa inaweza kufikia mara mbili ya fedha zinazokusanywa kwa sasa ambazo ni Milioni 500 kwa mwezi huku akiwataka Madiwani hao kupitia na kusimamia kila chanzo cha mapato ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na hatamvumilia yeyote atakayekwamisha makusanyo na kusababisha hoja za ukaguzi.
Aidha, Serukamba ameelekeza kwamba Madiwani washirikiane na wakuu wa Idara ili kufunga hoja zilizobaki na kuhakikisha wanakutana kila mwezi kufanya uangalizi wa mashaka ya kibenki ‘Benk Reconciliation’ ili kuepuka kuzalisha hoja.
Hata hivyo ameagiza kuendela kuboresha hali ya usafi katika maeneo mbalimbali huku akimtaka kutungwa sheria ndogo ambazo zitawabana wanaotupa taka hovyo ikiwa ni pamoja na kutoza faini kubwa jambo ambalo litaongeza mapato ya Manispaa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amewataka kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha hazizalishi hoja.
RAS amewataka kuhakikisha kwamba wanaendelea kupunguza hoja kwa kuzifunga ambapo anaamini kwamba zitapungua hadi kufikia tatu ambazo ni za kisera.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.