Takwimu za wananchi wanaopata chanjo ya Uviko19 mkoani Singida zimeendelea kuongezeka kwa kasi kufuatia jitihada za utolewaji wa elimu na ushawishi kwa jamii kwa njia ya nyumba kwa nyumba.
Akiongea wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Afya ya msingi (PHC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa, RC Dkt. Binilith Mahenge amesema wiki mbili kabla ya kuanzishwa Mpango Shirikishi na Harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo ya Uviko 19 idadi ya watu waliokuwa wakijitokeza kuchanja ilikuwa 5800 mpaka 6000 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida kabla ya tarehe 22 Septemba mwaka huu.
Dkt. Mahenge amesema Mpango Shirikishi na Harakishi ambao uelimishaji ulikuwa unafanywa nyumba kwa nyumba ulianza tarehe 22 Septemba 2021 katika Halmashauri zote saba 7 za Mkoa wa Singida ambapo ulisaidia kuongezeka idadi ya watu wanochanja mpaka kufukia 11,847 ilipofika tarehe 5.10.2021 kwa Mkoa mzima.
Aidha Huduma ya mkoba na kliniki tembezi zimesaidia kuwafikia wananchi wengi katika minada mbalimbali mashuleni na maeneo ambayo hayakuwa na vituo vya kutolea huduma ya chanjo. Alibainisha Dkt. Mahenge.
Hata hivyo Dkt. Mahenge ametumia Kikao hicho kuendelea kuwaomba wadau na taasisi mbalimbali kusaidia upatikanaji wa usafiri wa kuwafikisha watoa huduma ya chanjo vijijini ili kuendeleza kutoa Kinga ya ungonjwa huo.
Amewataka wahudumu wa Afya na watumishi mbalimbali wanaohamasisha jamii kuhusu kuchanja na kuendeleza kufanya hivyo Mara kwa Mara kwa kuwa wananchi wanakawaida ya kusahau.
Pamoja na mambo mengine wadau walikuwepo katika mkutano huo wamemuomba RC kushirikiana na wadau mbalimbali na mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea kusaidia mapambano dhidi ya Ugonjwa huu.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victorina Ludovick katika taarifa yake amesema kikao kilichopita waliadhimia kuendelea kutoa elimu ya chanjo na namna ya kujikinga na Ugonjwa wa Uviko 19.
Dkt. Ludovick amebainisha kwamba wataendelea kuwatumia viongozi wa dini na wanasiasa katika kupambana na Ugonjwa wa Uviko 19 kwa kuwa imeonekana kukubalika zaidi katika jamii zinazowazunguka.
Aidha uuzaji holela wa barakoa umeendelea kufanyiwa kazi hasa katika maeneo ya karibu na hospitali ambapo wapo wanaojaribisha kwa kuvaa barakoa hizo kabla ya kununua hivyo kuweza kusababisha maambukizi. Alisema Victorina Ludovick.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani hapa Mhe. Sophia Mfaume Kizigo amewataka wataalamu hao wa Afya kuongeza jitihada katika kutoa elimu maeneo ya mijini kwakuwa idadi kubwa ya waliochanja ipo Vijijini na sio mjini.
Hata hivyo DC huyo alitoa wito kwa kila mwananchi aliyepata chanjo kuwa balozi wa kusaidia uhamasishaji kwa wengine.
Mwisho.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.