• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

TEHAMA Chanzo Cha Mabadiliko Ya Uchumi - Dc Singida

Posted on: July 22nd, 2021

Mifumo ya TEHAMA imetajwa kuongeza makusanyo ya fedha za Serikali katika Wilaya ya Singida kutoka shilingi bilioni 1.98 mwaka 2014/15 mpaka shilingi bilioni 4.01 mwaka 2021 ambapo Wilaya ina mashine 280 za kukusanyia mapato.

Akiongea Julai 22, 2021 Katika hospitali ya St. Carolus Mtinko wakati wa uzinduzi wa mradi wa matumizi mbalimbali ya TEHAMA uliozinduliwa na mbio za Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili amesema matumizi ya Mifumo ni muhimu katika kuokoa muda na kuinua uchumi wa watu na Taifa kwa ujumla.

Amesema kwamba, kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2021 “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; Itumike kwa usahihi na uwajibikaji” imeakisi hali halisi ya miradi ya wilayani hapo ambapo mifumo imekuwa ikitumika kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha Mhe. Mhandisi Muragili amebainisha kwamba mifumo hiyo imechangia   Utumishi wa umma kuwa rahisi ikilinganishwa na awali ambapo kwa sasa imekuwa ikitumika katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii na utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na watumishi.

Naye  Afisa TEHAMA Bw. Joseph Micka Joseph amezitaja baadhi ya mifumo inayotumika kuwa ni mfumo wa bajeti (Planrep), mfumo wa taarifa za Watumishi  na Mishahara (Lowson –HCMIS), ukusanyaji wa mapato (LGRCIS), utunzaji wa taarifa za wagojwa (GoT- HoMIS) mfumo wa kiuhasibu katika utoaji wa huduma (FFRS), Taarifa za shule (SIS) mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi ( SAFARI), mfumo wa malipo (EPICOR- MUSE) na mfumo wa barua pepe.

Kwa upande mwingine Mwenge wa Uhuru 2021 umezindua mradi wa lishe bora katika kata ya Ilongero ambapo  wilaya imejivunia kupunguza idadi ya  watoto wenye utapiamlo kutoka watoto 22,854 kwa mwaka 2019/2020 hadi  kufikia 18,215 mwaka 2021 kwa watoto chini ya miaka 5.

Aidha Afisa lishe wa mradi huo Bi. Asha Mahami  amesisitiza kwamba uhamasishaji wa matumizi ya lishe bora yamefanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano 20 na vikao 32 vya wazazi na walezi katika vijiji na mitaa 61 na kata 31, lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto anapata lishe bora kwa siku 1,000 za mwanzo.

Aidha miradi mingine ni malaria uliopo kata ya Mtinko mradi wa maji  katika shule ya sekondari ya Itaja, ujenzi wa tenk la maji , Maabara na jengo la uthibiti wa ubora wa elimu lililopo  Manispaa ya Singida.

Mwenge wa Uhuru 2021 ukiwa Unawaka, Unang'ara na Kumelemeta ndani ya Wilaya ya Singida katika Miradi mbalimbali ya maendeleo   

Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Singida wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Maji wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2021

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi (kulia)  akipokea risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili wakati wa sherehe za Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021

HABARI PICHA ZAIDI BONYEZA; singidars.blogspot.com

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.