• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

TUENDELEE KUTENDA MEMA HATA BAADA RAMADHANI

Posted on: March 25th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amewaasa waumini wa dini ya kiislamu kuhakikisha matendo mema yanakuwa sehemu ya maisha yao na wala sio kutenda mema katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani pekee.

            Ameyasema hayo wakati wa kupata ifutari pamoja na waumini wa dini ya kiislamu iliyoandaliwa Katika kuunga mkono mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani katika Kiwanda cha kuchambua pamba cha Bioustain  mkoani Singida, wakifuturisha waumini wa Kiislamu na wananchi wengine waliojumuika pamoja.

Akizungumza katika iftari hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuweza kufuturisha, huku akisema kitendo hicho kinampendeza mwenyezi Mungu kwa kuonyesha ishara ya mshikamano na upendo kwa Waislamu na jamii kwa ujumla.

      "Sadaka kama hizi ni jambo la heri, mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitolea kwa ajili ya wenzao wengi, na bila shaka, huu ni mfano wa kuigwa," alisema Mheshimiwa Dendego.

Katika hatua nyingine,  Mhe.Dendego, amewakumbusha Wananchi kutumia vizuri sherehe za mei mosi, zitakazofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Singida akisema sherehe hizo ni fursa adhimu kwa wananchi wa mkoa wa Singida, kwani kwa muda wa wiki mbili mkoa utapokea zaidi ya wageni 6,000, ambao watahitaji huduma mbalimbali, ikiwemo chakula na malazi.

              "Hii ni nafasi nzuri kwa wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kuweza kujiandaa ipasavyo, ili wanufaike kiuchumi...tuitumie vyema fursa hii kwa kuongeza kipato chetu, na kuboresha maisha ya familia zetu," alisisitiza Dendego.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issah Nassoro, ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa waumini wa Kiislamu na jamii kwa ujumla, kuendelea na mwenendo mzuri hata baada ya Ramadhani.

                "Tusirejee kwenye dhuluma na maovu, naomba wafanyabiashara wazingatie njia halali za kutafuta riziki, huku nao watumishi wa umma watosheke na mishahara yao, badala ya kujihusisha na vitendo vya rushwa, amesema.

       Aidha, Sheikh Nassoro ametangaza kuwa Swala ya Idd El-Fitr kwa mkoa wa Singida mwaka huu itafanyika kwenye viwanja vya Bombadia, huku akiwataka waumini wa Kiislamu kujitokeza kwa wingi kusali pamoja akisema ni vyema waumini waendelee kudumisha mshikamano na kujihusisha na ibada, hata baada ya Ramadhani, huku akitoa mfano wa namna mwezi mtukufu unavyoleta mabadiliko chanya katika jamii.

           Matendo mema, uadilifu na mshikamano ni nguzo muhimu si kwa mwezi wa Ramadhani pekee, bali kwa maisha ya kila siku, na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha thamani ya mfungo wa mwezi mtukufu, inakuwa sehemu ya maisha ya kudumu.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.