• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Tushirikishe viongozi katika utekelezaji wa miradi ya TASAF - RC. Mahenge

Posted on: May 28th, 2022

Ushirikishwaji mdogo wa Viongozi wa Wilaya na Wakurugenzi wa  Halmashauri katika utekelezaji wa miradi ya TASAF  kunasababisha miradi hiyo kutokamilika kwa wakati na kushindwa kufikia malengo yalikusudiwa.

Waratibu wa TASAF katika ngazi za Wilaya hawatoi taarifa kwa viongozi wao na kwa Wakurugenzi wa  Halmashauri badala yake wanatuma taarifa moja kwa moja kwa waratibu wa kitaifa jambo ambalo limekuwa likiongeza changamoto za kiusimamizi.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge alipohudhuria mafunzo ya mifumo mbalimbali ya uendeshaji miradi ya TASAF yaliyofanyika katika Hotel ya KBH iliyopo mjini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na Viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri (hawapo pichani) waliohudhuria mafunzo ya mifumo mbalimbali ya uendeshaji miradi ya TASAF.

RC Mahenge amebainisha kwamba katika miradi hiyo kuna fedha zinazotolewa kwa ajili ya ufuatiliaji lakini viongozi hawawezeshwi jambo ambalo limekuwa likisababisha miradi kutopata usimamizi unao stahili.

“Ipo miradi ya kijamii kama mabwawa au malambo ambapo kulihitaji kuongezewa nguvu kidogo na Halmashauri kwa kuwa baadaye watachukua ushuru na ajira kwa watu hao zingeongezeka na  wangehitimu mapema" alisema RC Mahenge.

Serikali inatoa fedha nyingi  katika miradi ya TASAF ambazo kama wakiachiwa waratibu peke yao kuna uwezekano mkubwa wa malengo kutofikiwa hivyo niwaombe wakuu wa Wilaya  msaidie kusimamia ili wananchi waweze kunufaika.

Akimalizia hotuba yake Mkuu wa Mkoa amewataka waratibu kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi kuhusiana na uendeshaji wa Miradi hiyo kwa kuwa jamiii imekuwa na maswali mengi hasa katika ajira za muda na namna ya ulipaji wa fedha zao.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu ameipongeza Serikali kwa kuongeza idadi za wanufaika katika miradi hiyo huku akibainisha uwepo wa changamoto kadhaa za kimfumo zikiwemo baadhi ya wanufaika kukosa sifa kwa sababu ya kuwa viongozi na kuomba jambo hilo liweze kuangalia vizuri.

Mafunzo yakiendelea

Katika Mafunzo hayo yaliwahusisha wenyeviti wa Halmashauri ambao kwa nyakati tofauti nao walionesha baadhi ya changamoto katika maeneo na kuomba TASAF makao makuu kuangalia namna ya kuzitatua.

Awali akitoa taarifa ya Mradi wa TASAF awamu ya pili Kaimu Meneja wa malipo kwa walengwa na uhaulishaji fedha Kitaifa Msangi Tsetonga amebainisha kwamba  Mradi una gharama ya Dola za Kimarekani 883.31 sawa na Trilioni 2.03 ambayo ni sawa na asilimia 0.5 na walengwa ni Milioni 1.45 ambao utambuzi ulifanyika katika Vijiji zaidi ya 6000.

Bwana Msangi amesema tathmini inaonesha kwamba kuna Kaya zenye uwezo wa kufanya kazi zipatazo 979,918 sawa na asilimia 67 wakati familia zenye uwezo wa kufanya kazi lakini hazina watoto ni 190,988 sawa na asilimia 13.2 ki Taifa. 

Mratibu huyo akabainisha kwamba jumla ya Kaya 179,821 sawa na asilimia 12.4 ni Kaya za wazee walemavu na wagonjwa wa muda mrefu na hazina watoto.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na wakuu wa Wilaya wenyeviti wa Halmashauri Wakurugenzi wakuu wa Idara na waratibu wa Mradi.


MATUKIO KATIKA PICHA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu (kushoto) pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya wakishiriki Mafunzo hayo.

Sehemu ya Sekretarieti ya Mkoa wa Singida wakishiriki Mafunzo hayo.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.